Maana ya Kufunga
Ni mjumuisho wa mambo haya matatu:
Kuomba – Isaya 58:4 ..ni kuisikizisha sauti yetu juu
Kujuta na kuacha dhambi na pia kusamehe yote na kutoa sadaka kwa wasiojiweza mfano:Isaya 58: 5 …kutafuta kukubaliwa na Bwana
Isaya 58: 6 – 7… Kufungua vifungo vya uovu, Kuwaacha huru walioonewa, Kuwagawia wenye njaa chakula chako, Kuvunja kila nira, Kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako,Kuwavika nguo wasio nazo nk
Kuacha yale uyapendayo, yaliyo muhimu kwako mfano chakula, burudani au sherehe badala yake kusoma sana Neno na kulitafakari mfano:
2 Nyakati 7:14…. Ikiwa vatu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekeza mbele zangu na kuutafuta USO WANGU….
Danieli 10:2 ni kuomboleza … mimi Danieli nalikuwa nikiomboleza ktk majuma matatu kamili, sikula chakula kitamu wala nyama wala divai…
Esta 4: 16 ….mkafunge kwa ajili yangu, msile wala kunywa muda wa siku tatu……
2 Samweli 12: 16 Basi Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya mtoto, Daudi akafunga, akaingia akalala chini usiku kucha…
Kufunga sio mashindano na ugomvi au kujiona bora kuliko wasiofunga Isaya 58: 4 na pia kutega kazi au kuwaelemea wengine na kuwa mvivu Isaya 58: 3
3. Faida za Kufunga
Kusikiwa na Mungu katika shida, maafa mfano: Esta 4, Isaya 58:9 ndipo utaita na Bwana ataitika, utalia atasema Mimi hapa!
Kufunuliwa maono mfano Danieli 10:1 …Danieli ambaye jina lake aliitwa Belteshaza alifunuliwa neno, na neno lile lilikuwa kweli….
Kuponywa au kuponya magonjwa, vifungo na kuwa na afya njema mfano
Isaya 58:7, 11 ….afya yako itatokea mara, Mathayo 17 20 -21 …halitakuwepo neno lisilowezekana kwenu, …Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga
Kupokea ulinzi wa Mungu daima: Hutodhulumiwa, kuonewa, mfano
Isaya 58: 8 Kupokea haki zako, kupokea ulinzi na utukufu wa Mungu kuonekana kwako
Kuwa na amani na mleta amani kwa watu, kanisa na kuwarudisha watu kwa Mungu, mfano Isaya 58: 12 .. …utaitwa mwenye kujenga palipobomoka, mwenye kurejesha njia….utaiinua misingi ya vizazi vilivyoanguka
2Nyakati 7:14 ….basi nitasikia kutoka mbinguni na kusamehe dhambi zao na kuiponya nchi yao pia
Esta 5:6 Basi mfalme akamwambia Esta pale kwenye karamu, dua yako ni nini utapewa hata nusu ya Ufalme
Kupokea nguvu na uwezo kwa Roho Mt, mfano Isaya 58: 11 Bwana atakuongoza daima…utakuwa kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
Matendo 13: 2 Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana Ibada na kufunga, Roho Mt akasema nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.
Uwezo wa kushinda majaribu kupitia uongozi wa Roho Mt: Luka 4: 1 na Yesu hali amejaa Roho Mt, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho Mt muda wa siku arobaini nyikani akijaribiwa na ibilisi, na siku hizo alikuwa hali kitu….
Utainuliwa na kubarikiwa sana mfano Isaya 58:14 nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka, nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako…
Aina za kufunga
Siku 40+ (kadri Roho atakavyokuongoza hizi ni funga za muda mrefu ni Mungu aliewaongoza)
Kwa ajili ya toba, kuwaleta watu kwa Mungu au kupeleka Injili mfano;
Luka 4:1 – 14 …(baada ya kufunga siku 40) …Yesu akarudi kwa nguvu za Roho Mtakatifu, akaenda Galilaya, habari zake zikaenea kwa watu wote, akifundisha ktk masinagogi yao akitukuzwa na watu wote.
Torati 9:1-18 Musa kuileta torati kwa Waisraeli, na pia kutubu kwa ajili yao walipomkosea Mungu …….Torati 9: 18 Nikaanguka nchi mbele za Bwana siku 40, usiku wala mchana sikula chakula wala kunywa maji, kwasababu ya makosa yenu yote mliyokosa, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana….
Siku 21(masaa 12 kavu au kupunguza baadhi ya vyakula)
Kwa ajili ya mafunuo au maono:
Danieli 10: 1 ….alifunuliwa neno, na neno lile ni vita vikubwa naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo.
Siku 1 – 3 (Kavu au maji tu)
Kuomba kuondolewa Shida (crisis), vifungo, kupokea utakaso, ulinzi wa Mungu, kupata kusikilizwa shida zako.
Esta 4: 16 ….mkafunge kwa ajili yangu, msile wala kunywa muda wa siku tatu……
2 Samweli 12: 16 Basi Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya mtoto, Daudi akafunga, akaingia akalala chini usiku kucha…
Hitimisho:
Kama una ugonjwa wowote au unakunywa dawa tafadhali shauriana na Dr aina ya kufunga, lakini kwa Mkristo wa kawaida ni vizuri kufunga walau siku 1 kwa wiki ili kujitakasa, kupokea ulinzi wa Mungu, kupokea uwezo wa Roho Mt na kusikiwa ktk haja zako. Kwa walio ktk huduma au utumishi walau funga ya siku 3 mara moja kwa mwezi ni muhimu ili uweze kuhudumu vema na sio Mkristo kusubiri hadi shida au ugonjwa, crisis ndo unaanza kufunga, matatizo yanatakiwa yakukute na kugonga mwamba, kila mara tunafunga kujiweka imara.
Haya ni jinsi Roho alivyonifundisha kuna aina nyingi na faida nyingi tunaweza ziongezea hapa ili tujifunze zaidi, lakini cha muhimu ni kuwa ni Roho ndiye atuongozaye ktk jinsi na muda wa kufunga. Ubarikiwe sana namuomba Mungu akujalie uwezo wa kufunga ukiongozwa na Roho Mtakatifu ktk Jina la Yesu. Amen.
No comments:
Post a Comment