Sunday, February 3, 2013

MATUKIO YA KICHAWI (sehemu ya pili)

UTANGULIZI:
Watu wengi wanajiuliza kwanini
tunazungumzia uchawi mara nyingi, hii ni
kwasababu shetani hutumia wachawi
katika kutenda kazi duniani; na ndio
maana katika Biblia kuna maandiko
mengi yanayotaja uchawi na wachawi
kama ifuatavyo:- Hesabu 23:23 24:1;
1Wafalme 9:22; 2Wafalme 17:17;
Isaya 47:9,12; Mika 1:12; Nahumu
3:4; Matendo ya Mitume 8:9; 18:11;
Wagalatia 5:20; 3:1; Ufu 9:21. Ni kweli
tumepewa mambo yote na Mungu kama
vile afya na mafanikio lakini shetani
kupitia wachawi amekuwa akizuia, hivyo
tunatakiwa kushughulika nao katika
ulimwengu wa roho.. Katika sehemu ya
kwanza ya somo hili tuliona kwa habari
ya Ayubu ambapo shetani alipata ruhusa
ya kugusa maisha yake. Shetani
hakumtokea Ayubu kwa namna ambayo
angemfahamu kuwa ni shetani, lakini
alimjia kwa njia ya matukio, kumbe
waweza kuwa unapitia kwenye hali
mbaya kumbe ni matukio
yanayosababishwa na wachawi.
Wakristo walio wengi wanapambana na
shetani bila kujua nguvu za adui wanae
pamaba nae. Nchi ya Japani ilipokuwa
haijui kuwa Marekani wana bomu la
nyuklia; waliwachokoza wakidhania kuwa
watashinda, Lakini matokeo yake
walishindwa kwasababu walikuwa
hawajui nguvu ya wanayeshindana naye.
Mara nyingi watu wengi hupambana na
shetani bila kujua nguvu zake na
matokeo yake wengi huishia kushindwa.
Huwezi kupambana na adui usiyemjua,
vivyohivyo ili uweze kumshinda shetani
ni lazima uanze kwa kutafuta maarifa
kuhusu yeye.
MAFURIKO YA KICHAWI:
Ufunuo 12:13-16 Yule Joka alikuwa
shetani, Biblia inasema Yule joka akatoa
maji kama mto; kwa kawaida
ingeonekana kama mafuriko ya maji
dhidi ya yule mwanamke. Kumbe kuna
matukio yanaweza kutokea kwenye
maisha yako au kwenye nchi, na kumbe
yamesababishwa na wachawi. Si kila
moto au mafuriko ni ya kiasili, mengi
huwa yanasababishwa na shetani ili
kuua watu ili awashushe kuzimu. Kuna
matukio yanatokea unadhania kuwa ni
ya kawaida kumbe yameletwa na
wachawi ili kuangamiza watu. Ni
muhimu kujifunza kuyaangalia matukio
kwa jicho la rohoni.
BIASHARA ZA KICHAWI:
Ezekieli 28:16, 18. “kwa wingi wa
uchuuzi wako; watu walikujaza
udhalimu” shetani mfanya biashara naye
hutenda kazi pamoja na wachawi na
waganga wa kienyeji. Kwa njia hii
shetani anafunga maisha ya watu, na
ndio maana kuna watu wanafanya
biashara za kichawi, Yaani
wanamwendea shetani halafu
wanamuomba aiwezeshe biashara yao
kwa kumpa shetani ama damu au
kafara. Wachawi wanapokuwa wanatoa
kafara, huwa wanakuwa wanafanya
biashara na shetani. Ufunuo 18:1-
mstari 5” “wafanya biashara wa nchi
wamepata mali kwasababu ya kiburi
chake” mstari 11” “nao wafanya
biashara wa nchi walia na kuomboleza
maana hapana mtu anunuaye bidhaa zao
tena” mstari 13 ” biashara ya roho na
miili ya wanadamu. Kumbe biashara
nyingi unazoona watu wanafanya
duniani, ni biashara za kichawi. Yaani
mtu anafanya biashara lakini ndani yake
kuna uvuvio wa kishetani, Nahumu 3 : 4 .
Ndio maana biashara za watu wengi
hazifanikiwi wakati huohuo watu
wanaomtegemea shetani wanafanikiwa
kwa haraka ni kwasababu wameuza roho
zao kwa shetani.
Matendo ya Mitume 16:16-17; 19:24
“aliyewapatia bwana zake faida nyingi”
biashara hizi zipo kabisa, na ndio maana
unaweza kufanya biashara lakini
wenzako wanauza zaidi kuliko wewe
hata kama wote mnauza bidhaa ileile,
kumbe wenzako wamenuiza ili wao
wauze na wewe usiuze. Ni vizuri kuanza
kufanyabiashara na BWANA, yaani kabla
ya kuanza biashara ni muhimu kufanya
maombi kwanza ili kuiweka biashara
yako katika ulinzi wa Mungu. Unapotaka
kuanza biashara fanya na BWANA.
MAGONJWA YA KISHETANI:
Kuna watu ni wagonjwa sasa kwasababu
ya wachawi. Magonjwa mengi sana
husababishwa na wachawi. Unaweza
kuwa unasumbuliwa na magonjwa
yasiyopona kwasababu ya chanzo chake
ni cha rohoni. Na ndio maana
unapooumwa hata kama utaenda
hospitali unatakiwa usiache maombi
kwasababu shetani anaweza kusababisha
magonjwa, hata Ayubu aliumwa majipu
mabaya ambayo kimsingi yalisababishwa
na shetani.
BIBLIA NA MATUKIO YA KICHAWI:
Mathayo 9:32 “tazama walimletea mtu
bubu mwenye pepo, na yule pepo
alipotolewa alinena” huyu ni mtu
ambaye watu walipomuangalia
walimuona ni bubu. Cha ajabu Yesu
alipomuona hakushughulika na ububu
bali alishughilika na pepo kuonyesha
kwamba ule ububu ulisababishwa na
pepo. Kuna mambo mengi ambayo
yanasababishwa na shetani, hivyo
unatakiwa kuyashughulikia.
Mathayo 13:10-15 “alikuwa na pepo wa
udhaifu kwa muda wa miaka kumi na
nane…” 15” “na huyu mwanamke aliye
uzao wa Ibrahimu ambaye shetani
shetani amemfunga” watu walishamzoea
kumwona kuwa ni mama mwenye
kibiyongo yaani hawezi kujinyoosha
kabisa lakini Yesu alipomtoa pepo Yule
mama alipona.
Wachawi wapo na watu wengi
wanalogwa, Kumbukumbu la Torati
18:11 ; watu wanalogwa na wanalogeka,
matatizo ya watu wengi yanasababishwa
na shetani kupitia matukio ya kichawi.
Marko 9:17 ; kuna magonjwa ambayo
yanakuja kwenye maisha ya mtu
kwasababu ya kulogwa. Katika utendaji
kazi wa shetani anaweza akaingia ndani
ya mtu na kumfunga, lakini pia shetani
anaweza kumkandamiza mtu akiwa nje
ya mwili na ndio maana kwa watu
waliokoka lakini hawapigani vita ya
rohoni wanaweza kujikuta
wanakandamizwa na shetani akiwa nje
yao. 1Wathesalonike 2:18 , Paulo
hakuwa amepagawa na pepo lakini
shetani alimzuia. Zekaria 3:1 . Shetani
anaweza kukuzuia kutokea nje, yaani
unahitaji kwenda nje ya nchi lakini
shetani anakuzuia kupitia mtoa pasi ya
kusafiria. Matendo ya Mitume 13:6
hata wachawi hupambana pia ili
kukuzuia, ni muhimu kuishi maisha huku
ukijua kunakushindana rohoni.
JINSI YA KUSHINDA DHIDI YA
MATUKIO YA KICHAWI
Mpokee Yesu kwanza; huwezi
kushindana na shetani kama hujaokoka,
ni muhimu umpokee Yesu kwanza ili
akuwezeshe kupigana katika vita dhidi ya
shetani. Jifunze kuomba mwenyewe;
baada ya kuokoka kuna amani ya
mwanzo unayoipata ile isikufanye
ukasahau kuwa tupo vitani, kama
tulivyoona hapo juu wanaoshindana
nawe wanaweza kuwa ndani yako au nje
yako. Katika hali hiyo unachotakiwa
kufanya ni kujifunza kuomba mwenyewe
kwasababu hata ukitegemea kuombewa
kila siku, kuna muda utakuwa
mwenyewe, na hapo unatakiwa
usimame mwenyewe. Mtu uliyeokoka
unatakiwa uhame kwenye ule wokovu
wa kuombewa uhamie kwenye wokovu
wa maarifa na kupambana kwa kutumia
Jina la Yesu Kristo.

No comments:

Post a Comment