BWANA YESU ASIFIWEE.......
Nakukaribisha mpendwa katika Kristo
Yesu,tujifunze kwa pamoja kuuhusu
ujumbe huu wa leo,Na umekujia muda
sahihi kabisa ungali U mzima wa afya.
Nependa kutambua uwepo wa Roho
mtakatifu muda huu,Ninamualika Yeye
Roho wa Bwana achukue nafasi,ashuke na
uweza wake ili uelewe pindi usomapo
ujumbe huu,maana Yeye ndie mwalimu
wetu siku ya leo.
Hayo maneno yaliyobeba kichwa cha somo
letu ni maneno ya Bwana Yesu Kristo
alipokuwa anawaambia wanafunzi wake, Na
ni maneno ya msingi katika mchakato wa
kwenda mbinguni,Sasa twaweza kusoma ;
Mathayo 18 : 1-3
“ Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu
wakisema,
Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa
mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka
katikati yao,
akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka
na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe
katika ufalme wa mbinguni. ”
Waingiao katika ufalme wa mbinguni ni
wale wenye kufanana kama watoto
wadogo,maana hawa watoto siku zote wao
ni wanyenyekevu sana.
Kumbuka ;
Bwana Yesu Kristo alikuwa anaongea na
wanafunzi wake,wale ambao waliitao Jina
lake,wenye hofu na Mungu,Labda kwa leo
niseme Yesu anazungumza na wewe
uliyeokoka akikuambia USIPOONGOKA NA
KUWA KAMA MTOTO
MDOGO,HAUTAINGIA KAMWE KATIKA
UFALME WA MBINGUNI..
Yaani ingawa umeokoka lakini bado
kuokoka kwako hakukusaidii kuingia katika
ufalme wa mbinguni kama usipoongoka.
• JE KUONGOKA NI NINI ?
• JE KUNA TOFAUTI GANI KATI YA
KUONGOKA NA KUOKOKA ?
MAJIBU ;
Kuongoka ni kugeuka kwa mwenendo wako
wa kwanza na kufuta mwenendo mpya
baada ya kusikia neno la Mungu.
Tofauti kati ya kuongoka na kuokoka ni hii;
• Kuongoka sio NEEMA ya Mungu kwa yule
aliyeongoka,Bali ni jitihada zake pindi
anapoukulia wokovu. Baada ya kuokoka.
• Bali Kuokoka ni KIPAWA/NEEMA ya
Mungu mwenyewe kwa watu wake, Hapa
tunasoma Waefeso 2 : 8-9
“ Kwa maana mmeokolewa kwa neema,
kwa njia ya imani; ambayo hiyo
haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha
Mungu;
wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije
akajisifu. ”
Haleluyaa…
Sasa unaweza ukawa umeokoka lakini
haujaongoka,Yaani umepewa neema ya
kumkiri Bwana Yesu Kristo, kuwa Bwana na
mwokozi wa maisha yako,na kuitwa
MLOKOLE katika jamii ulipo werwe,
lakini ujabadilika matendo yako yale ya
mwanzo kabla ya kuokoka yaani kama ni
WIZI unaufanya kidogo chini kwa chini,au
kama ni UZINZI pia unaufanya chini kwa
chini,na MTU YEYOTE WA NAMNA
HII,HUYO BADO HAJAONGOKA NA KAMWE
HATAINGIA KATIKA UFALME WA
MBINGUNI.
Mfano wa kuongoka;
Tumtizame mtume Paulo namna
alivyokuwa kabla ya kuongoka;
MATENDO 22 : 1-4
“ Enyi wanaume, ndugu zangu na baba
zangu, nisikilizeni, nikijitetea mbele yenu
sasa.
Waliposikia kwamba anasema nao kwa
lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza;
akasema,
Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso,
mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu,
miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria
ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa
jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote
mlivyo leo hivi;
nikawaudhi watu wa Njia hii hata kuwaua,
nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume
na wanawake. ”
Hapo Paulo anasimulia kwa kujitetea
akiwaambia Wayahudi namna
alivyokuwepo hapo awali,lakini pindi
alipookolewa na Bwana Yesu na kutengwa
kwa dhumuni maalumu la kuwa mtume na
mjumbe wa Yesu Kristo,Ndipo
akaongoka,yaani akabadili ule mwenendo
wake wa awali wa kuwahudhi wakristo,na
kuwa mpya kwa ajili ya kazi ya Bwana.
Sasa siku hizi kuna kundi kumbwa la watu
waliokoka kama fasion lakini
HAWAJAONGOKA NA KUWA KAMA
WATOTO WADOGO na watu hayo
nawatangazia kwamba HAWATAUONA
UFALME WA MBINGUNI.
JE NI KWA NINI BWANA YESU ATUMIE
MFANO WA WATOTO KATIKA KUONGOKA?
MAJIBU ;
Kwa sababu watoto wadogo ni wale wenye
KUTII ,na sifa kama,na kuwa na sifa kama
zifuatazo ;
• Watoto wadogo usikia na kushika kile
wanachoambiwa bila kuhoji hoji
• Watoto wadogo hucheza na wenzao kwa
kushirikiana bila kuulizana kabila zao wala
hata majina yao .MFANO ;
wanapocheza wote wanakuwa ni wamoja
watoto wa masikini na watoto wa tajiri
huwezi kuwatofautisha pindi wachezapo.
• Hawapendi makuu,MFANO UNAWEZA
KUMWAMBIA SHUKA KWENYE KOCHI NA
UKAE CHINI,NAYE HUKAA MUDA ULE ULE.
• Watoto wadogo HUPENDANA wana
upendo mzuri
• Hawashikilii mambo Mfano WANAWEZA
KUGOMBANA WAO KWA WAO NA GAFLA
UKIPITA MUDA MDOGO TU,WANAKUWA
PAMOJA WAKICHEZA hawashikilii hasira.
• Watoto wadogo wana DHAMILI
SAFI,ISIYOKUWA NA HATIA Mfano MTOTO
WA KIKE ANAWEZA KULALA MPAKA
ASUBUHI NA MTOTO WA KIUME BILA
KUFANYA CHOCHOTE TENA HATA
WAKILALA UCHI,AU HATA KAMA
WATAKWENDA KUOGA PAMOJA WAO NI
SAWA TU maana dhamila zao zi safi mbele
za Mungu. N.K
Sasa mtu asipo GEUKA na kuwa na TABIA
kama hizo za watoto wadogo KAMWE
HAWEZI KUINGIA KATIKA UFALME WA
MBINGUNI.
JE WEWE UME UKOKA NA KUONGOKA ?
-Au umeokoka bila kuongoka ?
-Au umengoka bila kuokoka ?
Watu wa DINI wao wanaweza kuwa
wameongoka,na kufuata amri na sheria za
dini zao lakini HAWAJAOKOKA na hawana
mpango wowote wa kuokoka na
wakijidanganya kuwa DINI zao kwamba
zitawapeleka mbinguni,au kwa kuongoka
kwao,
Mimi leo ninakutangazia Kuongoka kwa
DINI yako KAMWE HAKUKUINGIZI
MBINGUNI BILA KUOKOKA
KWANZA,ukishaokoka ndipo mchakato wa
kuongoka unafuata.
Na yule aliyeokoka ,asipoongoka KAMWE
HAWEZI KUINGIA KATIKA UFALME WA
MBINGUNI
Mfano ;
Tazama wanafunzi wa Yesu ,wao walokuwa
wameshaokoka,Lakini bado Yesu Kristo
anawaambia na kuwasisitiza WAONGOKE.
( Mathayo 18 : 1-3 )
Haleluyaaa..
Kumbuka ;
Mchakoto wa kwenda mbinguni kwanza
UOKOKE kisha ufanye kuukulia wokovu
yaani KUONGOKA
Ukishaokoka ndipo unafanya mazoezi ya
kugeuka kabisa kwa mwenendo wako wa
kwanza na hapo ikiwa utafanya hiyo
utafanana na mtoto mdogo.
NI OMBI LANGU KWAKO,
KWAMBA KUONGOKA /KUBADILI
MWENENDO WAKO WEWE WENYEWE
HAUWEZI BILA MSAADA WA YESU KRISTO
ULLIYEMPOKEA,
SASA UMSIHI SANA MUNGU AKUPE
UJASIRI NA UWEZO KUACHA KILA JAMBO
BAYA NAYE ATAKUGEUZA UWE MALI
YAKE .
UBARIKIWE.
No comments:
Post a Comment