Tuesday, February 5, 2013

MAOMBI YANAYOZAA MATUNDA

Na-
MCHUNGAJI: FRANK ANDREW (RP)

UTANGULIZI:

Mungu anatuhitaji tuombe, tunatakiwa
tuombe sio tu kwasababu tunauhitaji
bali kwasababu Mungu anahitaji tuombe.
Tatizo la watu wengi wanashindwa
kupokea majibu ya maombi
wanayoomba na wengine wameshindwa
hata kuomba.wengine wamejikuta
wakikata tama bila kujua kuwa wao ndio
wanakosea katika kupeleka haja zao kwa
Mungu na katika kupokea. Hapa
tutajifunza sababu na jinsi ya kuomba ili
kupokea kutoka kwa BWANA.

SABABU NNE: KWANINI
TUNAMUOMBA MUNGU:

1. Kujinyenyekesha mbele za Mungu.
2. Kuonyesha kuwa yeye ni Mungu
wetu.
3. kuonyesha kuwa vyote viko mikononi
mwake
4. Tunampa heshima kama baba
mwenye familia ya watoto watakatifu.

MAOMBI YANAHUSISHA VITU
VIKUBWA VITATU:

1. Mhusika AU muombaji mwenyewe:-
huyu ndiye muombaji na mwanzilishi wa
maombi.
2. Maombi yenyewe:- haya ni mahitaji
au ujumbe ambao unapelekwa kwa
unaye muomba.
3. Unayemuomba:- unayemuomba ni
nani kwako na mna uhusiano gani naye.
Kwa kujua umuhimu wa kuomba,
wanafunzi wa Yesu walimwomba Yesu;
awafundishe jinsi kuomba na hapo Yesu
aliwapa fomula ya kuitumia ili kuomba.
Hii ndiyo inayoitwa sala ya BWANA,
kimsingi hii ni kanuni ya kuomba
aliyoifundisha Yesu na si maombi
yenyewe kama wengi wanavyodhani,

KANUNI hii ni sawa na kanuni yengine za
kufanya jambo fulani. Mfano kuna
kanuni za kupika au kanuni za kuimba.
Tatizo la watu wengi ni kwamba
wanatumia hii kanuni kama ndio
maombi yenyewe. Kwa mfano Yesu
aliposema “Baba yetu uliye mbinguni…”
alimaanisha kuwa unapokuwa unaanza
kuomba ni lazima ujue unamuomba
baba aliye mbinguni na si magomeni. Hii
ni kanuni jinsi ya kuomba na haitaji moja
kwa moja haja yako, bali ukiitumia kama
kanuni inakuletea majibu:=

Yakobo 5: 15-16 “kuomba kwake
mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa
bidii”, Biblia inaposema kuomba kwake
mwenye haki: anamaanisha kuwa yeye
anayeanzisha maombi ni lazima awe ni
mwenye haki yaani msafi. Kiukweli kuna
wakati mwingine Mungu hutenda
kwasababu ya neema yake lakini
kimsingi ili maombi yako yafae inabidi
uwe mwenye haki. Hivyo kabla ya
kuingia kwenye maombi unatakiwa
ujitakase kwanza ili Mungu akikutazama
aone uko safi. Ni muhimu kutengeneza
uhusiano mzuri na Mungu, tengeneza
haki kwanza kabla ya kuingia kwenye
maombi. Yaani kama hujaokoka uokoke
kwanza, na kama umeokoka lakini hauko
sawa na Mungu, unatakiwa utengeneze
maisha yako kwanza. Katika mstari wa
15* Biblia inasema “ungameni dhambi
zenu ninyi kwa ninyi” ikiimaanisha kuwa
kabla ya kuingia kwenye maombi
unatakiwa ujisafishe na ujitakase
kwanza.
Baada ya kujitakasa kinachofuata ni
kupeleka ujumbe wenyewe kwa Mungu.
Watu wengi kwasababu hukosea kuomba
wamedhania kuwa Mungu huwa hajibu
maombi; lakini Biblia inasema Mungu
anajibu maombi. Biblia inasema, Zaburi
2:8 “uniombe nami nitakupa mataifa
kuwa urithi wako...” na katika Mathayo
7:7 “Ombeni nayi mtapewa…” kumbe
unapoomba lazima Mungu akujibu kama
ukiomba sawasawa na mapenzi yake. Ni
muhimu kabla ya kupeleka hoja yako
uamini kwanza kuwa Mungu yupo
sawasawa na Waebrania 11:6 “...lazima
aamini kuwa Mungu yupo”. Haya
maandiko tutatumia katika kuangalia
jinsi ya kuomba na wapi watu wengi
wanapokosea wakiwa katika kuomba…

KANUNI ZA KUPOKEA KUTOKA KWA
MUNGU:

Watu wengi wanajua kuomba lakini kati
yao wengi hawajajua namna ya kupokea.
Kwasababu kuna namna ya kuomba na
namna ya kupokea. Watu wengine
wanajua kuomba lakini hawajui jinsi ya
kupokea haja zao. Haifaidii kitu kujua
kuomba na huku ukiwa hujui jinsi ya
kupokea. Kuna mambo kadhaa ambayo
unatakiwa uyatilie maanani unapokuwa
unaomba kama ifuatavyo:-

1. Tengeneza uhusiano wako na
Mungu:-
Maandiko yanasema “haja zenu na
zijulikane mbele za Mungu” pamoja na
kuwa Mungu anajua haja zetu lakini bado
anahitaji sisi tumuombe. Hii ni sawa na
kuomba kwa jirani wakati baba yako
mzazi yupo; utajisikiaje mtoto wako
anapokuwa na shida alafu akuombi
wewe baba yake, alafu yeye
anajitengenezea sanamu na kuiomba.
Utakavyojisikia ni sawa kabisa na Mungu
anavyojisikia kwetu ndio maana Mungu
anasema kuwa anaona wivu (kutoka
20:4) . Mungu anataka tumuombe yeye
ili kujenga uhusiano na yeye. Ukiomba
au kuiabudu sanamu unamfanya Mungu
awe na wivu.

2. Unaongea nini ukiwa katika
maombi yako:-
Maombi unayoongea kwenye maombi ni
ya muhimu sana kwenye kupokea haja
zako kutoka kwa BWANA. Ttuangalie
kwa habari ya Hana; 1Samweli1:1-24; Elikana alikuwa na wake wawili
Penina na Hana, kama lilivyojina lake
Hana hakuwa na watoto kwasababu
tumbo lake lilikuwa limefungwa. Hana
hapo kwanza alikuwa anaenda na
malalamiko na kulia. Watu wengi
hupeleka malalamiko kwa BWANA,
badala ya kupeleka hoja kwa Mungu.
Hata siku moja Mungu atendi jambo bila
kusudi, na ndio maana tumbo la Hana
lilikuwa limefungwa kwa muda wote ule.
Emu tuangalie mambo kadhaa
yaliyokuwa yakimzuia Hana.
>Sababu ya kuomba:-
1Samweli 1:1-24 Hana alikuwa
anamuomba Mungu ampe mtoto ili
amkumeshe penina, na ndio sababu
inayowafanya wengi washindwe kupokea
kwa BWANA kwasababu hawana sababu
ya Kibiblia inayowafanya Mungu awape
mahitaji yao. Mfano mtu anamwomba
Mungu mke ili amfulie nguo au
amechoka kuishi mwenyewe. Hiyo si
sababu; Mungu anahitaji hoja yenye
nguvu ili upokee mwambie jukumu lako
la kutimiza kwenye maisha yako na
nafasi ya mke katika kumtumikia Mungu;
hapo lazima akutendee.

>Peleka haja ya moyo wako:-

Mungu haitaji hali yako ikoje sasa bali
anahitaji kujua unataka nini. Picha ya
tatizo lako unatakiwa uwe nayo wewe
lakini mbele za Mungu unatakiwa
upeleka haja ya moyo wako na si
malalamiko. Kwa wakati ule Hana
alikuwa anapeleka hali yake ilivyo na
penina na si uhitaji wake kwa BWANA.
Unakuta mtu anamuomba Mungu gari ili
awaonyeshe wengine, huyo hawezi pata
kwasababu si sawa na mapenzi ya
Mungu.

>Mwangalie Mungu na si jambo
unalohitaji:

Ibarahimu alipompokea Isaka
ilimradhimu Mungu kumjaribu ili ajue
upendo wake upo kwa Isaka au kwa
Mungu. Watu wengi wanamuomba
Mungu jambo lakini wakilipokea ndilo
linalofanyika mzigo mkubwa wa
kutokumtumikia Mungu, mfano mtu
anaomba mume akipokea tu; baada ya
siku chache haji kanisani anasema eti
anamuhudumia mumewe. Kwasababu
hii hata Hana akupata mtoto mpaka
alipobadilisha maombi na kumuomba
Mungu mtoto, kwa kumuahidi BWANA
kumtoa mtoto huyo awe mtumishi
wake.

3. Imani na Bidii:
Watu wengi wanafikiri bidii ni kutumia
nguvu tu katika maombi, bali bidii ni ule
mzigo; ni muhimu unapokuwa unaomba
uwe na mzigo wa kuombea. Ili uzae
matunda katika maombi ni lazima uwe
sawa na mama mjauzito aliye katika
kuzaa; lazima uwe na uchungu yaani
umaanishe. Vivyohivyo kupokea kutoka
kwa BWANA Unatakiwa umaanishe na
lazima uamini pia kuwa ni wakati wako
wa kupokea kutoka kwa BWANA.
Unapoomba unatakiwa moyo na akili
yako iwe kwenye kile unachohitaji. Kuna
watu wanabidili maombi kila kukicha kwa
kuhisi kuwa Mungu awasikii lakini bidii ni
kubaki kwenye jambo hilo hadi uone
amani moyoni kuwa BWANA
ameshatenda na hili jambo ndilo ambalo
Eliya alilifanya alipokuwa anaomba mvua
kunyesha tena. Eliya alikuwa
mwanadamu wa namna moja na sisi
alikuwa na Bidii katika maombi.

JAMBO LA KUFANYA:

Baada ya kujua mambo haya ni muhimu
kubadili mtazamo wako na jinsi
unavyoomba. Mungu anajibu maombi
kama ukiomba sawasawa na neon lake.
Kwanza uwe na picha ya kile ambacho
unataka BWANA akutendee, uombe na
imani na bidii. Hapo lazima Mungu
akutendee kwasababu hakuna baba
ambaye mwanaye atamwomba mkate
akampa jiwe au samaki akampa nyoka.
Badili mtazamo wako katika maombi
yako ili uwe mpokeaji wa maombi yako
ni si mwombaji asiyepokea chochote!!!

-FRANK ANDREW-
Resident Pastor G.C.T.C

1 comment:

  1. UBARIKIWE SANA KAKA KWA HABARI HII NJEMA SANA NA HAKIKA NIMEBARIKIWA SANA NA UJUMBE WA SOMO HILI PIA NIMEJIFUNZA KITU

    ReplyDelete