Na:- SOSPETER SIMON S. NDABAGOYE.
BWANA Yesu asifiwe sana,
Napenda kumshukuru Mungu
kwaajili yako unaesoma ujumbe huu.
Ndugu Msomaji, naomba
nikukaribishe katika somo letu la
leo, linalohusu juu ya KUOGOPA
KULIPIZA KISASI.
Dhana ya Kisasi inaweza kutazamwa
kama hali ya kiushindani baina ya
pande mbili zinazokinzana hususani
pale upande mmoja unapokuwa
umeonewa au haujatendewa haki.
Maandiko yanasema: "Kulipiza kisasi
ya paswa tumwachie
Mungu" (Warumi 12:19 ) "Wapenzi
sijilipizie kisasi bali ipisheni
ghadhabu ya Mungu maana
imeandikwa kisasi ni juu yangu
mimi; mimi nitalipa anena Bwana."
Pia, ( Mithali 20:22) Yasema,
"Usiseme mimi nitalipa mabaya
mgojee Bwana naye atakuokoa."
Tusilipize kisasi kwa ajili ya upendo.
Hatahivyo,(Mathayo 5:38-39 )
inasisitiza "Mmesikia kwamba
imenenwa jicho kwa jicho na jino
kwa jino LAKINI MIMI NAWAMBIA
msishindane na mtu mwovu lakini
mtu akupigaye shavu la kuume
mgeuzie la pili."
MANENO HAYANATUONYA JUU YA
KUWA WAVUMILIVU NA
KUCHUKULIANA HUKU
TUKIOMBEANA NA KUSAMEHEANA.
Mungu anajua kuwa kuudhiana na
kuoneana kupo, ila ametuonya kuwa
wavumilivu na kutotaka kuchukua
hatua wenyewe kwa wenyewe bali
tumwache aingilie kati mwenyewe.
Hata hivyo, anatuonya tusishangilie
pale wenzetu waingiapo matatizoni
hata kama ni adui zetu.
Biblia inasema "Usifurahi adui wako
anapo kuwa na taabu" (Mithali
24:17-18) "Usifurahi adui wako
aangukapo wala moyo wako
usishangilie ajikwaapo Bwana asije
akaliona hilo likamkasirisha
akageuza mbali naye hasira yake."
NAOMBA NIWASIHI NDUGU ZANGU,
KUJICHUKULIA MADALAKA
MKONONI, HATA KAMA TUMEKERWA
NI KINYUME NA MATAKWA YA
MUNGU KWETU.EBU TAFAKARI,
MTOTO WAKO NYUMBANI KAMA
AKIVUNJA KIKOMBE AU CHUPA YA
CHAI, UNAWEZA KUCHANA NGUO
YAKE AU KUVUNJA KITANDA CHAKE?
Je, inakuwaje wewe unaeamua
kumuua mwenzio au vinginevyo eti
kwa kile kinachosemwa eti kumalizia
hasira, kwani wote si wana wa
Mungu?
Naomba nichukue fursa hii
kuwaonya wote wanaoshiriki kwa
namna yoyote iwe kwa nguvu
binafsi, nguvu ya dola na hata
mahakama, kuwa kwa kulipiza kisasi
Unashiriki dhambi ya mtuhumiwa,
Kumbuka Neno la Mungu linasema
"USIHUKUMU USIJE
UKAHUKUMIWA"tena linaongeza,
Auaye kwa upanga naye atauawa kwa
Upanga, na hii ndiyo maana hata
Mahakama, inakusanya Wazee wa
Baraza ili Hakimu aivue laana hiyo
nakuwatwika wazee wa Baraza. Hata
Pilato, alisema Mimi nimenawa, na
ndipo Wayuda wakasema na Damu
yake iwe juu yetu na watoto wetu,
hii ina maana kuwa hata kama Yesu
angekuwa na makosa!Pilato hakuwa
tayari juu ya Kisasi cha Wayahudu
waliomshitaki Yesu licha ya kuwa
alijua kuwa hana hatia.
Naomba niwashauli ndugu zangu,
damu inayomwangwa kwaajili ya
kisasi chochote kile itakulilia wewe
na kizazi chako, vilio vya Yatima,
wana wake wanaoachwa na
wapendwa na wao na machozi yao
yote, yatakufuata wewe
uliyeyasababisha. Naomba unielewe
vizuri hapa, kuwa yale matatizo
yanayowakumba watu kutokana na
kisasi chako, ni juu yako.
Mungu atusaidie Watanzania
wenzangu, Mungu atusaidie wote
watu wa Mungu, kwani hali
tuliyonayo sii nzuri.
MUNGU AWABARIKI NA
KUWAONGOZA KATIKA MAAMUZI
YENU WOTE.
Ee Bwana fufua kazi yako katika Miaka.....Mungu awe nanyi nyote mnaposoma ujumbe huu ufanyike kuwa msaada na balozi mwema wewe kama Mkristo yaani uliye na Kristo ndani yako.AMEN
ReplyDeleteamen.....MUNGU azidi kuwafunulia zaidi sana
ReplyDelete