Sunday, November 4, 2012
NINAWEZAJE KUJUA KAMA NITAKWENDA MBINGUNI?
Ninawezaje kujua kwakweli nitaenda Mbinguni wakati nikifa?
Swali:
"Ninawezaje kujua kwakweli nitaenda Mbinguni wakati nikifa?"
Jibu:
Je, unajua kwakweli kua unauzima wa milele na utaenda Mbinguni wakati ukifa? Mungu anataka uwe na uhakika!
Bibilia inasema:
“Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue yakuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini jina la mwana wa Mungu” (1Yohana 5:13). Kama ungelikuwa umesimama mbele za Mungu saa hii na akuulize, “Kwanini nikuruhusu uingie Mbinguni?” Je, ungelisema nini? Unaweza usijue utajibu nini. Unachohitaji kujua nikwamba Mungu anatupenda na amepeana njia ambapo tunaweza kujua kwakweli ni wapi tutaishi milele.
Bibilia inasema hivi “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee,bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). Mwanzo kabisa ni sharti tuelewe shida ambayo inatupinga kufika Mbinguni. Shida ni hii- dhambi yetu ya asili inatupinga kuwa na uhusiano na Mungu. Sisi ni wenye dhambi kiasili na kwa chaguo. “Kwasababu wote wamefanya dhambi,na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Hatuwezi kujiokoa sisi wenyewe. “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zetu, ni kipawa cha Mungu. Wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu” (Waefeso 2:8-9). Tunastahili mauti na jehanamu. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23). Mungu ni mtakatifu na mwenye haki na nisharti aadhibu dhambi,kisha anatupenda na amepeana msamaha kwa ajili ya dhambi zetu. Yesu alisema “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima. Mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi’’ (Yohana 14:6). Yesu alitufia pale msalabani “Kwa maana Kristo naye alikufa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki,ili atulete kwa Mungu’’ (1Petro 3:18). Yesu alifufuliwa kutoka kwa wafu “Alitolewa kwa ajili ya makosa yetu nakufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki” (Warumi 4:25).
Sasa turudi kwa swali la kwanza –
“Ninawezaje kujua kwakweli nitaenda Mbinguni wakati nikifa?’’
Jawabu ni -
Mwamini Bwana Yesu Kristo nawe utaokoka (Matendo 16:31). Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12). Unaweza kupokea uzima wa milele kama karama ya bure. “Karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Bwana wetu’’ (Warumi 6:23). Unaweza kuishi maisha yenye ukamilifu na yenye maana sasa hivi. Yesu alisema mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” (Yohana 10:10). Unaweza kuishi maisha ya milele na Yesu Mbinguni. “Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi,nanyi mwepo” (Yohana 14:3).
Ukiwa unataka kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wako na upokee msamaha wa dhambi toka kwa Mungu, hapa kuna ombi unaweza kuomba.
Kwa kuomba ombi hili au ombi lengine lolote lile haitaweza kukuokoa.
Nikwakumwamini Yesu Kristo pekee ndiko kutakuwezesha kupokea msamaha wa dhambi.
Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kupeana kwa ajili ya msamaha wako.
“Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu ile niliyostahili ili kwa kumwamini yeye nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako ya ajabu na kwa msamaha! Amina!"
Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa?
Swali:
"Nimeweka imani yangu kwa Yesu … sasa ni fanyeje?"
Jibu:
Hongera! Umefanya uamuzi wa kubadilisha maisha!
Huenda ikawa unauliza, “sasa ni fanye nini? Nianze vipi safari yangu na Mungu?” Hatua tano zilizo orodheshwa hapo chini zitakupatia muongozo kutoka kwa Bibilia. Iwapo una maswali safarini mwako,tafadhali tembelea http://www.gotquestions.org/Kiswahili/sasa-ni-fanyeje.html
1. Hakikisha unaelewa maana ya wokovu.
1Yohana 5:13 anatuambia,” Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue yakuwa mna uzima wa milele. Mungu anataka tuelewe maana ya wokovu.Mungu anataka tuwe na ujasiri wa kufahamu kwa kweli kwamba tumeokoka. Kwa ufupi tu,wacha tuviendee vipengele muhimu vya wokovu: (a) Sote tumefanya dhambi.Sote tumefanya mambo ambayo hayampendezi Mungu (Warumi 3:23). (b) Kwasababu ya dhambi zetu,tunastahili kuadhibiwa kwa kutengwa milele na Mungu (Warumi 6:23). (c) Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu (Warumi 5:8; 2 Wakorintho 5:21).Yesu alitufia pahali petu,kwa kuchukua adhabu ambayo sisi tulistahili. Kufufuka kwake kulidhihirisha yakuwa kifo chake Yesu kilitosha kutulipia dhambi zetu. (d) Mungu hutoa msamaha na wokovu kwa wote wale wamuaminio Yesu – kwa kuamini kifo chake kama malipo ya dhambi zetu (Yohana 3:16; Warumi 5:1; Warumi 8:1). Hizo ndizo habari za wokovu! Ikiwa umeweka imani yako kwa Yesu kama mwokozi wako, umeokoka! Dhambi zako zote zimesamehewa na Mungu ana ahidi kutokuacha wala kutokutenga (Warumi 8:38;Mathayo 28:20).Kumbuka,wokovu wako uko salama ndani ya Yesu Kristo (Yohana 10:28-29). Ukiwa unamuamini Yesu pekee kama mwokozi wako, unaweza kuwa na uhakika yakuwa utaishi milele na Mungu mbinguni!
2. Tafuta Kanisa Zuri linalo fundisha Bibilia.
Usilifikirie Kanisa kama jengo.Kanisa ni watu. Ni muhimu sana kwa wamuaminio Yesu kristo kushirikiana mmoja na mwengine. Hiyo ndiyo sababu ya kwanza muhimu ya Kanisa. Sasa kwa kuwa umeweka imani yako kwa Yesu Kristo, tunakuhimiza vilivyo kutafuta Kanisa linalo amini mafundisho ya Bibilia katika eneo lako na uzungumze na Mchungaji. Mfahamishe upya wa imani yako katika Yesu Kristo. Sababu ya pili ya Kanisa, ni kufundisha Bibilia.Unaweza kujifundisha jinsi yakuyatumia maagizo ya Mungu katika maisha yako. Kulielewa Bibilia ni ufunguo wa kuishi katika ushindi na nguvu/ uthabiti katika maisha ya kikristo. 2Timotheo 3:16-17 yasema “kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho,na kwa kuwaonya watu makosa yao,na kwa kuwaongoza,na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.” Sababu ya tatu ya Kanisa ni kuabudu.Kuabudu ni kumshukuru Mungu kwa yote aliyo fanya!Mungu ametuokoa. Mungu anatupenda.Mungu anatutimizia mahitaji yetu. Mungu anatuongoza na kutuelekeza. Je ni kwanini tusingemshukuru? Mungu ni mtakatifu, mwenye haki,upendo,huruma na amejaa neema.Ufunuo wa Yohana 4:11 asema, “umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwasababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.”
3. Jitengee muda kila siku wa kutafakari juu ya Mungu.
Ni muhimu sana kwetu kuwa na mda wa kutafakari juu za Mungu kila siku. Wengine huuita” wakati wa kutafakari, wengine huuita wakati wa “kujitoa” kwasababu ni wakati tunapo jitolea kwa Mungu. Wngine hupendelea wakati wa asubuhi na wengine jioni. Haijalishi unauitaje wakati huu ama ni lini hujitoa. Kinacho stahili ni kwamba uwe na wakati na Mungu mara kwa mara. Ni matendo gani yanadhihirisha wakati wetu na Mungu?
(a) Maombi.
Maombi ni hali ya kuzungumza na Mungu. Kuongea na Mungu kuhusu hali zako na shida zako.Muulize Mungu akupe hekima na muongozo. Muulize Mungu akutane na mahitaji yako. Mwambie Mungu ni kwa jinsi gani unampenda na ni kwa kiwango gani unamshukuru kwa yale yote anayo kutendeaHiyo ndiyo maana halisi ya maombi.
(b) Kusoma Bibilia.
Zaidi ya kufundishwa Bibilia kanisani,katika shule ya Jumapili, na au kwa mafundisho ya Bibilia - unahitaji kujisomea Bibilia mwenyewe. Bibilia iko na kila kitu unacho hitaji kujua ili kukuwezesha kuishi maisha ya kikristo yenye ushindi. Ina muongozo wa kiungu katika hali yakufanya maamuzi ya hekima, katika hali ya kujua mapenzi ya Mungu, katika hali ya kuwahudumia wengine, na katika hali ya kukua kiroho. Bibilia ni neno la Mungu kwetu sisi. Bibilia ni muongozo muhimu wa Mungu katika hali ya kuishi maisha yanayo mpendeza ye (Mungu) na kututosheleza sisi.
4. Jenga uhusiano na watu watakao kusaidia kiroho
1Wakorintho 15:33 yasema, “Msidanganyike; mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.” Bibilia iko na tahadhari kuhusu ushawishi “mbaya” watu wanaweza kuwa nao juu yetu. Kutumia wakati na wale ambao wanajihusisha katika vitendo hivyo. Tabia za wale ambao tuko nao zitatuambukiza. Hii ndiyo sababu yakuwa ni muhimu tutangamane na watu wanao mpenda Bwana na wana wajibika kwake. Jaribu kutafuta rafiki mmoja au wawili, labda kwa kanisa yako, ambao wanaweza kukusaidia na kukutia changamoto (Waebrania 3:13;10:24). Waulize rafiki zako wakuajibishe kuhusu wakati wako wa kutafakari, matendo yako na mwenendo wako na Mungu. Uliza kama unaweza kuwafanyia hivyo pia. Hii haimaanishi yakuwa uwachane na marafiki zako wote ambao hawajamjua Yesu Kristo kama mwokozi wao. Endelea kuwa rafiki yao na uwapende. Kwa ufupi wafahamishe yakuwa Yesu amebadilisha maisha yako na huwezi kuyafanya tena yote, yale uliyo kuwa ukiyafanya. Muulize Mungu akupe nafasi ya kumshiriki Yesu pamoja na marafiki zako.
5.Batizwa (Ubatizwe)
Watu wengi wanakosa kufahamu maana ya ubatizo.Neno “ Kubatiza” inamaanisha kuzamisha au kutosa majini.
Ubatizo ndiyo njia ya kibibilia ya kujitambulisha hadharani imani yako mpya ndani ya Kristo na jukumu lako la kumfuata yeye. Kitendo cha kuzamishwa ndani ya maji inamaanisha kuzikwa pamoja na Kristo. Kitendo cha kutoka ndani ya yale maji inadhihirisha kufufuka kwa Kristo. Kubatizwa ni kujitambulisha wewe mwenyewe na kifo cha Yesu,maziko na ufufuo (Warumi 6:3-4). Ubatizo sio ukuokoao.Ubatizo haukuondolei dhambi zako. Ubatizo ni hatua tu ya utiifu, hali ya kujitambulisha hadharani kuhusu imani yako ndani ya Kristo pekee kwa wokovu. Ubatizo ni muhimu kwasababu ni hatua ya utiifu-hadharani ukijitambulisha imani yako ndani ya Kristo na jukumu lako kwake yeye. Kama uko tayari kubatizwa,zungumza na Mchungaji.
Tuesday, October 30, 2012
KUOGOPA KULIPIZA KISASI
Na:- SOSPETER SIMON S. NDABAGOYE.
BWANA Yesu asifiwe sana,
Napenda kumshukuru Mungu
kwaajili yako unaesoma ujumbe huu.
Ndugu Msomaji, naomba
nikukaribishe katika somo letu la
leo, linalohusu juu ya KUOGOPA
KULIPIZA KISASI.
Dhana ya Kisasi inaweza kutazamwa
kama hali ya kiushindani baina ya
pande mbili zinazokinzana hususani
pale upande mmoja unapokuwa
umeonewa au haujatendewa haki.
Maandiko yanasema: "Kulipiza kisasi
ya paswa tumwachie
Mungu" (Warumi 12:19 ) "Wapenzi
sijilipizie kisasi bali ipisheni
ghadhabu ya Mungu maana
imeandikwa kisasi ni juu yangu
mimi; mimi nitalipa anena Bwana."
Pia, ( Mithali 20:22) Yasema,
"Usiseme mimi nitalipa mabaya
mgojee Bwana naye atakuokoa."
Tusilipize kisasi kwa ajili ya upendo.
Hatahivyo,(Mathayo 5:38-39 )
inasisitiza "Mmesikia kwamba
imenenwa jicho kwa jicho na jino
kwa jino LAKINI MIMI NAWAMBIA
msishindane na mtu mwovu lakini
mtu akupigaye shavu la kuume
mgeuzie la pili."
MANENO HAYANATUONYA JUU YA
KUWA WAVUMILIVU NA
KUCHUKULIANA HUKU
TUKIOMBEANA NA KUSAMEHEANA.
Mungu anajua kuwa kuudhiana na
kuoneana kupo, ila ametuonya kuwa
wavumilivu na kutotaka kuchukua
hatua wenyewe kwa wenyewe bali
tumwache aingilie kati mwenyewe.
Hata hivyo, anatuonya tusishangilie
pale wenzetu waingiapo matatizoni
hata kama ni adui zetu.
Biblia inasema "Usifurahi adui wako
anapo kuwa na taabu" (Mithali
24:17-18) "Usifurahi adui wako
aangukapo wala moyo wako
usishangilie ajikwaapo Bwana asije
akaliona hilo likamkasirisha
akageuza mbali naye hasira yake."
NAOMBA NIWASIHI NDUGU ZANGU,
KUJICHUKULIA MADALAKA
MKONONI, HATA KAMA TUMEKERWA
NI KINYUME NA MATAKWA YA
MUNGU KWETU.EBU TAFAKARI,
MTOTO WAKO NYUMBANI KAMA
AKIVUNJA KIKOMBE AU CHUPA YA
CHAI, UNAWEZA KUCHANA NGUO
YAKE AU KUVUNJA KITANDA CHAKE?
Je, inakuwaje wewe unaeamua
kumuua mwenzio au vinginevyo eti
kwa kile kinachosemwa eti kumalizia
hasira, kwani wote si wana wa
Mungu?
Naomba nichukue fursa hii
kuwaonya wote wanaoshiriki kwa
namna yoyote iwe kwa nguvu
binafsi, nguvu ya dola na hata
mahakama, kuwa kwa kulipiza kisasi
Unashiriki dhambi ya mtuhumiwa,
Kumbuka Neno la Mungu linasema
"USIHUKUMU USIJE
UKAHUKUMIWA"tena linaongeza,
Auaye kwa upanga naye atauawa kwa
Upanga, na hii ndiyo maana hata
Mahakama, inakusanya Wazee wa
Baraza ili Hakimu aivue laana hiyo
nakuwatwika wazee wa Baraza. Hata
Pilato, alisema Mimi nimenawa, na
ndipo Wayuda wakasema na Damu
yake iwe juu yetu na watoto wetu,
hii ina maana kuwa hata kama Yesu
angekuwa na makosa!Pilato hakuwa
tayari juu ya Kisasi cha Wayahudu
waliomshitaki Yesu licha ya kuwa
alijua kuwa hana hatia.
Naomba niwashauli ndugu zangu,
damu inayomwangwa kwaajili ya
kisasi chochote kile itakulilia wewe
na kizazi chako, vilio vya Yatima,
wana wake wanaoachwa na
wapendwa na wao na machozi yao
yote, yatakufuata wewe
uliyeyasababisha. Naomba unielewe
vizuri hapa, kuwa yale matatizo
yanayowakumba watu kutokana na
kisasi chako, ni juu yako.
Mungu atusaidie Watanzania
wenzangu, Mungu atusaidie wote
watu wa Mungu, kwani hali
tuliyonayo sii nzuri.
MUNGU AWABARIKI NA
KUWAONGOZA KATIKA MAAMUZI
YENU WOTE.
Sunday, October 28, 2012
MKARIBISHE YESU KWENYE CHOMBO CHAKO.
Mathayo 14:22-33, Yesu alikuwa akiendelea kutenda kazi alizokuja kuzifanya duniani na ukisoma kuanzia Mathayo 14:1-… Utaona aliwalisha watu elfu tano (waume). Na wakati watu wakitaamaki akawalazimisha wanafunzi wake kupanda chomboni ili wavuke bahari. Wanafunzi wake walipokuwa katikati ya bahari ndipo ilipotokea upepo mkali na kuanza kusukasuka chombo. Tuna mambo mengi ya kujifunza kupitia maandiko haya:-
HALI YA WANAFUNZI KATIKA CHOMBO:
Ukitafakari kwa makini utaweza kuona hali ya wanafunzi chomboni; inawezekana walishaanza kumlaumu Yesu, au kumlaumu kwa kuwalazimisha kupanda chomboni na yeye asiwemo.
Pia, wanafunzi wa Yesu walikuwa wamekata tama, kwasababu tukio hili lilipotokea mwanzo walikuwa na Yesu chomboni akaukemea upepo lakini mara hii Yesu hakuwepo chomboni. kwa maana hiyo wanafunzi walikuwa katika hofu kuu.
Biblia inasema hata wanafunzi walipomuona Yesu akitembea juu ya maji, wakahisi ni kivuli chake. hapa tunajifunza kuwa kuna wakati kwenye maisha unaweza kuwa unapita kwenye hatua ngumu kimaisha, na kwasababu ya hofu ukajikuta unaiogopa njia ambayo ndio ufumbuzi wa tatizo lako.
KWANINI YESU ALITEMBEA JUU YA MAJI:
Yawezekana umejiuliza kwanini Yesu alikuja huku akiwa juu ya maji; Kimsingi bahari ndio ambayo ilikuwa tatizo kwa wanafunzi wake, kwahivyo Yesu alikanyaga bahari kuonyesha kuwa lile tatizo lilikuwa chini ya miguu ya Yesu. Kumbe Yesu yupo juu ya tatizo linalokuzunguka maana lipo chini ya miguu yake.
Na ndio maana Petro naye alijaribu kupita juu ya tatizo yaani bahari lakini alipoiangalia bahari alipata hofu. HAPA tunajifunza jambo kwamba hatakiwi kuliangalia tatizo bali mwangalie Yesu ambaye yupo juu ya tatizo.
Ukimwamini Yesu unavuka kutoka mautini unaingia uzimani, na Yesu ana mamlaka na funguo za mauti na kuzimu. Hivyo ukiwa kwenye tatizo, usiangalie tatizo bali mwangalie Yesu. unapoelekea kwa Yesu usipepese macho, mtazame Yesu aliyekufa msalabani kwaajili yako.
JAMBO LA KUFANYA UKIWA NDANI YA TATIZO:
Katikati ya bahari wanafunzi wakamuona Yesu kama tumaini lao, na ndipo Petro alipoamua kumfuata. kimsingi uamuzi wa Petro kumfuata Yesu kwa kutembea juu ya maji ni sahihi kabisa, ila tatizo ni kwamba petro alitumia uzoefu wake wa bahari ambao ukamfanya asiwaze sauti ya Yesu aliyemuita. watu wengi wameshindwa kutoka ndani ya tatizo kwasababu ya taarifa walizozisikia kutoka kwa watu.
Mfano; Mtu ana tatizo la ndoa na ndio limeanza, lakini baada ya kuongea na mtu mwengine mwenye tatizo kama hilo, anamwambia kuwa amedumu kwenye tatizo hilo kwa miaka mingi. Taarifa hiyo moja tu inamfanya huyu ambaye tatizo la ndoa ndio limeanza, akate tamaa na kuingiwa na hofu kabisa kwa kuhisi naye atadumu kwa miaka hiyo yote.
Ni muhimu kujua hakuna haja ya kuangalia tatizo wala watu wengine waliopo kwenye tatizo. tunatakiwa tumuangalie Yesu Kristo ambaye aweza kukutoa kwenye tatizo ulilonalo. unapomwita Yesu kwenye mwili wako uliojaa magonjwa atakapofika yeye yote yatakoma, ukimwita Yesu kwenye ndoa yako yenye matatizo atakapofika tatizo litakama.
Isaya 41:9-10 “wewe nilikushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia, Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa; usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwamaana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.” Kama ukijua jambo ambalo Mungu anataka utend kwenye tatizo utalibadili tatizo hilo na kuwa daraja la kukuvusha na kukupeleka kwenye hatma njema ya maisha yako.
Maombi:
Baba Mungu katika Jina la Yesu Kristo leo nimetambua kuwa ninatakiwa nitakiwa nikutazame wewe ninapokuwa kwenye tatizo. ninaomba msamaha kwasababu ya kutazama mambo mengine badala kukutazama wewe Mungu, Mungu naomba unisamehe katika Jina la Yesu.
Katika Jina la Yesu nimeamua kukuita wewe leo, imeandikwa katika Yeremia 3:33 “niite, nami nitakuitikia, name nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.” Leo ninakuita katika Jina la Yesu. Mungu kutoka katika kiti chako cha enzi ninakuita katika Jina la Yesu. Ninakutumaini wewe Mungu katika Jina la Yesu. Natakanivuke na wewe Mungu hadi ng’ambo ya maisha yangu katika Jina la Yesu.
MWITE YESU KWENYE TATIZO ULILONALO!!!
Saturday, October 27, 2012
JE UNAFAHAMU AHADI ZA MUNGU?
Ahadi za Biblia
Mungu hutimiza ahadi zake.
Imeandikwa katika 2Wakorintho 1:19-20 "Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu aliyehubiriwa katikati yenu na sisi yaani mimi na Silwano na Timotheo hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni Ndiyo.
Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa sisi."
Mungu hazirudishi ahadi zake au kuzibadilisha.
Imeandikwa katika Zaburi 89:34 "Mimi sitalihalifu agano langu, sitalibadili neno lililotoka mdomoni mwangu."
Hakuna mojawapo ya ahadi za Mungu ambazo hazijatimika.
Imeandikwa katika Yoshua 23:14 "Angalieni mimi nimekwenda njia ile waendayo watu wote wa ulimwengu...... Mungu wenu katika habari zenu yote yametimia kwenu hapana neno lo lote mlilopungukiwa."
Tumeahidiwa uzima wa milele.
Imeandikwa katika 1 Yohana 2:25 "Nahii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani uzima wa milele." Mungu aweza kufanya mambo yasiyowekana.
Imeandikwa katika Luka 18:27 "Akasema yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa mungu."
Tumeahidiwa moyo mpya na maisha mapya
Imeandikwa Ezekieli 36:26 "Mimi nitawapa moyo mpya nami nitatia roho mpya ndani yenu nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama."
Ametuahidi kutusamehe dhambi zetu.
Imeandikwa katika 1Yohana 1:9 "Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."
Ametuahidi tunda la roho. Imeandikwa katika Wagalatia 5:22-23 "Lakini tunda la roho ni upendo, furaha amani, uvumilivu, utu wema fadhili uaminifu, upole, kiasi juu ya mambo kama hayo hakuna sheria."
Ametuahi kututoa katika hofu. Imeandikwa katika Zaburi 34:4 "Nilimtafuta Bwana akanijibu, akaniponya na hofu zangu zote." Ameahidi wokovu. Imeandikwa katika Isaya 49:25, "... Kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu."
Ameahidi Roho mtakatifu Imeandikwa Luka 11:13 "Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho mtakatifu hao wamwombao?."
Atatutimizia mahitaji yetu. Imeandikwa katika Wafilipi 4:19, "Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu."
Hatatunyima lililo jema. Imeandikwa katika Zaburi 84:11 "Kwa kuwa BWANA, Mungu ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema hao waendao kwa ukamilifu."
Ametuahidi hekima. Imeandikwa katika Yakobo 1:5 "Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima na aombe dua kwa Mungu awapae wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa."
Mungu ametuahidi amani. Imeandikwa katika Isaya 26:3 "Utamlida yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini."
Mungu ametuahidi kutuepusha na majaribu. Imeandikwa katika 1Wakorintho 10:13 "Jaribu halikuwapata ninyi isipokuwa lililo kawaida ya binadamu; ila Mungu ni mwaminifu; hatawacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wakutokea ili muweze kustahimili."
Tumeahidiwa afya njema na tiba. Imo katika Biblia, Yeremia 30:17 "Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema BWANA..."
Mungu ameahidi kutulinda na hatari na ajali. Imeandikwa katika Zaburi 91:10 "Mabaya hayatakupata wewe, wala tauni haitaikaribia hema yako."
Biblia yatuahidi ya kwamba waliokufa watafufuka katika ufufuo. Imeandikwa katika Yohana 5:28-29 "Msistaajabie maneno hayo kwa maana saa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale walio fanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wao walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu."
Yesu ameahidi ya kwamba atarudi tena. Imeandikwa katika Yohana 14:2-3 "Nyumbani mwa Baba yangu kuna makao mengi; kama sivyo ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaanadalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu ili nilipo nanyi muwepo."
Ameahidi kukomesha vifo, maumivu na dhiki. Imeandikwa katika Ufunuo 21:4 "Naye atafuta kila chozi katika macho yao wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita."
Wednesday, October 24, 2012
RAINBOW SONG ~ LENNY LEBLANC
If I was a songbird I'd sing my song for You
And if You take the sun and the moon
Take away the stars at night
Your faithful Word will always be my light
Beautiful such a miracle
That You would give up Heaven just for me
All I wanna do is fall more in love with You
This world doesn't owe me anymore
And one thing that I do know for sure
Christian lyrics - RAINBOW SONG LYRICS - LENNY LEBLANC
Tuesday, October 23, 2012
KWANINI UITWE MKRISTO?
Wapendwa Bwana YESU KRISTO Asifiwe!
Napenda tushirikiane kwenye Mada hii ili tusaidiane kuelimishana katika safari hii ya Mbinguni,
Maana bila KUOMBEANA na KUELIMISHANA hatuwezi kuchuchumilia ile TAJI tuliyoahidiwa.
Haya tiririka Mpendwa!!!
Monday, October 22, 2012
MPENDWA UMEANDAAJE MAPITO YA BWANA?
Sunday, October 21, 2012
TAMBUA MAANA YA KUFUNGA
Ni mjumuisho wa mambo haya matatu:
Kuomba – Isaya 58:4 ..ni kuisikizisha sauti yetu juu Kujuta na kuacha dhambi na pia kusamehe yote na kutoa sadaka kwa wasiojiweza mfano:Isaya 58: 5 …kutafuta kukubaliwa na Bwana
Isaya 58: 6 – 7… Kufungua vifungo vya uovu, Kuwaacha huru walioonewa, Kuwagawia wenye njaa chakula chako, Kuvunja kila nira, Kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako,Kuwavika nguo wasio nazo nk
Kuacha yale uyapendayo, yaliyo muhimu kwako mfano chakula, burudani au sherehe badala yake kusoma sana Neno na kulitafakari mfano:
2 Nyakati 7:14…. Ikiwa vatu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekeza mbele zangu na kuutafuta USO WANGU….
Danieli 10:2 ni kuomboleza … mimi Danieli nalikuwa nikiomboleza ktk majuma matatu kamili, sikula chakula kitamu wala nyama wala divai…
Esta 4: 16 ….mkafunge kwa ajili yangu, msile wala kunywa muda wa siku tatu……
2 Samweli 12: 16 Basi Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya mtoto, Daudi akafunga, akaingia akalala chini usiku kucha… Kufunga sio mashindano na ugomvi au kujiona bora kuliko wasiofunga Isaya 58: 4 na pia kutega kazi au kuwaelemea wengine na kuwa mvivu Isaya 58: 3
3. Faida za Kufunga
Kusikiwa na Mungu katika shida, maafa mfano: Esta 4, Isaya 58:9 ndipo utaita na Bwana ataitika, utalia atasema Mimi hapa! Kufunuliwa maono mfano Danieli 10:1 …Danieli ambaye jina lake aliitwa Belteshaza alifunuliwa neno, na neno lile lilikuwa kweli…. Kuponywa au kuponya magonjwa, vifungo na kuwa na afya njema mfano
Isaya 58:7, 11 ….afya yako itatokea mara, Mathayo 17 20 -21 …halitakuwepo neno lisilowezekana kwenu, …Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga Kupokea ulinzi wa Mungu daima: Hutodhulumiwa, kuonewa, mfano
Isaya 58: 8 Kupokea haki zako, kupokea ulinzi na utukufu wa Mungu kuonekana kwako Kuwa na amani na mleta amani kwa watu, kanisa na kuwarudisha watu kwa Mungu, mfano Isaya 58: 12 .. …utaitwa mwenye kujenga palipobomoka, mwenye kurejesha njia….utaiinua misingi ya vizazi vilivyoanguka
2Nyakati 7:14 ….basi nitasikia kutoka mbinguni na kusamehe dhambi zao na kuiponya nchi yao pia
Esta 5:6 Basi mfalme akamwambia Esta pale kwenye karamu, dua yako ni nini utapewa hata nusu ya Ufalme Kupokea nguvu na uwezo kwa Roho Mt, mfano Isaya 58: 11 Bwana atakuongoza daima…utakuwa kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
Matendo 13: 2 Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana Ibada na kufunga, Roho Mt akasema nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Uwezo wa kushinda majaribu kupitia uongozi wa Roho Mt: Luka 4: 1 na Yesu hali amejaa Roho Mt, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho Mt muda wa siku arobaini nyikani akijaribiwa na ibilisi, na siku hizo alikuwa hali kitu…. Utainuliwa na kubarikiwa sana mfano Isaya 58:14 nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka, nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako…
Aina za kufunga
Siku 40+ (kadri Roho atakavyokuongoza hizi ni funga za muda mrefu ni Mungu aliewaongoza)
Kwa ajili ya toba, kuwaleta watu kwa Mungu au kupeleka Injili mfano;
Luka 4:1 – 14 …(baada ya kufunga siku 40) …Yesu akarudi kwa nguvu za Roho Mtakatifu, akaenda Galilaya, habari zake zikaenea kwa watu wote, akifundisha ktk masinagogi yao akitukuzwa na watu wote.
Torati 9:1-18 Musa kuileta torati kwa Waisraeli, na pia kutubu kwa ajili yao walipomkosea Mungu …….Torati 9: 18 Nikaanguka nchi mbele za Bwana siku 40, usiku wala mchana sikula chakula wala kunywa maji, kwasababu ya makosa yenu yote mliyokosa, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana….
Siku 21(masaa 12 kavu au kupunguza baadhi ya vyakula)
Kwa ajili ya mafunuo au maono:
Danieli 10: 1 ….alifunuliwa neno, na neno lile ni vita vikubwa naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo.
Siku 1 – 3 (Kavu au maji tu)
Kuomba kuondolewa Shida (crisis), vifungo, kupokea utakaso, ulinzi wa Mungu, kupata kusikilizwa shida zako.
Esta 4: 16 ….mkafunge kwa ajili yangu, msile wala kunywa muda wa siku tatu……
2 Samweli 12: 16 Basi Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya mtoto, Daudi akafunga, akaingia akalala chini usiku kucha…
Hitimisho:
Kama una ugonjwa wowote au unakunywa dawa tafadhali shauriana na Dr aina ya kufunga, lakini kwa Mkristo wa kawaida ni vizuri kufunga walau siku 1 kwa wiki ili kujitakasa, kupokea ulinzi wa Mungu, kupokea uwezo wa Roho Mt na kusikiwa ktk haja zako. Kwa walio ktk huduma au utumishi walau funga ya siku 3 mara moja kwa mwezi ni muhimu ili uweze kuhudumu vema na sio Mkristo kusubiri hadi shida au ugonjwa, crisis ndo unaanza kufunga, matatizo yanatakiwa yakukute na kugonga mwamba, kila mara tunafunga kujiweka imara.
Haya ni jinsi Roho alivyonifundisha kuna aina nyingi na faida nyingi tunaweza ziongezea hapa ili tujifunze zaidi, lakini cha muhimu ni kuwa ni Roho ndiye atuongozaye ktk jinsi na muda wa kufunga. Ubarikiwe sana namuomba Mungu akujalie uwezo wa kufunga ukiongozwa na Roho Mtakatifu ktk Jina la Yesu. Amen.
Wednesday, October 17, 2012
Je UNAYO HERI ???
Ana heri Mtu yule anisikilizaye, Akisubiri siku zote malangoni pangu Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.
Maana yeye Anionaye mimi aona UZIMA, Naye atapata kibali kwa BWANA.
Bali anikosaye hujidhuru nafsi yake mwenyewe, Na wao wanichukiao hupenda MAUTI.