Na Mch. Kiongozi: Josephat Gwajima
Jumapili 27 th
January 2013
Kuna matukio ambayo yanaweza
kutokea kwenye maisha yako na ukaona
kuwa ni kawaida, lakini tambua kuwa
matukio mengi huanzia rohoni. Matukio
ya kishetani yanayoanzia rohoni
yanaitwa matukio ya Kichawi. Tutajifunza
somo hili kwa kuangalia kwa undani
kuhusu Ayubu. Ayubu 1:1-... ; kitabu
cha Ayubu kinaanza kwa kusema
palikuwa na mtu mmoja katika nchi ya
Usi…. Ayubu alikuwa anamcha BWANA,
si mwenye dhambi…
Shetani akamwambia Mungu
umembariki Ayubu ndio maana
anakucha wewe, Mungu akamwambia,
Katika Mstari wa 12’ “tazama yote
aliyonayo yapo mikononi mwako lakini
usinyooshe mkono juu yake mwenyewe”
jambo la ajabu linatokea, mara tu baada
ya Mungu kumruhusu shetani, jambo la
kwanza shetani alianza kwa kuharibu
mali zake (Ayubu 1:13…). Na katika kila
tukio alilofanya shetani, alibakisha mtu
mmoja wa kumpelekea habari Ayubu.
Hii ni kwasababu shetani alitaka Ayubu
asijue kuwa ni shetani bali Waseba ndio
walioua na kuchukua mifugo wake ili
amuhamishe mtazamo asifahamu kuwa
ni jambo la kishetani,ndivyo amabavyo
shetani anatenda kazi ahata leo.
Tukio la kwanza, Ayubu 1:13-15 Waseba
waliwavamia watumishi wa Ayubu,
unaweza ukawachunguza Waseba katika
mitazamo miwili. Upande mmoja ni
kwamba waseba ni mashetani waliovaa
miili au ni watu walioingiliwa na mapepo
kuharibu wanyama wa Ayubu. Tukio la
pili limetajwa katika mstari wa 16’
kwamba moto ulishuka kutoka
mbinguni, mtoa taarifa anaita moto wa
Mungu, lakini katika kitabu cha (Ufunuo
13:13) inasema shetani anaweza
kushusha moto pia. Huyu mfanya kazi
aliita moto wa Mungu ili kwa njia hiyo
shetani amdanganye Ayubu aache
kuangalia shetani bali awaze kuwa ni
matukio ya kawaida kutokea. Ndio
maana katika waebrani 11:34 , biblia
inasema kwa imani walizima nguvu za
moto, kwasababu kuna moto ambao
waweza kuletwa na shetani. Haijalishi
unapitia moto gani kwenye maisha yako,
moto wa mikosi, kushindwa, umaskini na
kila moto wa maisha yako uzime katika
Jina la Yesu Kristo usiite ni matukio ya
asili.
Tukio la tatu linawahusu Wakaldayo,
katika mstari 17’ wameunda vikosi vitatu
vitatu, nao ni watu ambao
wameandaliwa na shetani ili kutekeleza
yale maongezi ya mwanzo ya Mungu na
shetani. Kumbe ni muhimu kuangalia
matukio kwa namna ya rohoni, liwe
tukio la kukosa umeme au nchi kuwa
maskini liangalie kwa namna ya rohoni.
Nguvu ya shetani ni kukufanya uwaze
kuwa ni tukio la kawaida au la kiasili
lakini kumbe kuna nguvu ya shetani
nyuma yake. Tukio la nne ni upepo
uliotokea na kuangusha nyumba
waliokuwepo watoto wa Ayubu
waliokuwa kwenye sherehe. Cha ajabu
ni kwamba watoto wote wa Ayubu
walikufa kwa maana ndio walikuwa
walengwa,ila Yule mtoa taarifa hakufa
kwasababu si mtoto wa Ayubu na pia
hakuwa amelengwa yeye. Kumbe
unaweza kuwepo mtego wa kichawi nao
unakuwa umemlenga mtu husika, na
ndio maana katika Biblia inataja mitego
ya ibilisi, yaani ibilisi anaweza kumtega
mtu katika kitabu 2Timotheo 2:26
“wapate tena fahamu zao, na kutoka
katika mtego wa ibilisi…..” hivyo alikuwa
anabakishwa mmoja kwasababu lile tego
halimuhusu, maana tego humlenga mtu
au watu husika.
Usione ni kawaida, matukio kama hayo
yanapotokea katika maisha yako, mfano,
unaanza saluni halafu haifanikiwi kumbe
ni kwasababu ya shetani, cha kufanya
unatakiwa uingie rohoni kushughulikia.
Pigo la Ayubu kubwa la kumwekea
majipu katika mwili na magojwa,
unaweza kuhangaika hospitali kama
hujajua kuwa kimeanzia rohoni, hospitali
wataita jipu au cancer lakini kumbe
limeanzia rohoni. Na ndio maana
unaweza kuona meli zinazama hadi
hazionekani kumbe ni kazi za adui
shetani, ni muhimu kujua kila unapoona
matukio duniani kuna matukio ya
kishetani ama yameletwa na shetani au
yamesukumwa kuwepo na shetani. Na
ndio maana ni muhimu unapoingia
kwenye hatari au ajali ukailiitia Jina la
Yesu ambalo ndilo pekee tulilopewa
kuokolewa kwalo.
1Thesalonike 2:18 “ Nalitaka kuja
kwenu….. lakini shetani akatuzuia”
shetani anaweza kumzuia mtu, na mara
nyingi kwenye kuzuia shetani hutumia
watu wa kawaida ili usimtambue.
Huwezi kukutana naye macho kwa
macho kwasababu anatumia waseba,
wakaldayo au upepo. Na ndio maana
unaweza ukawa unataka kusafiri lakini
ukazuiwa na mtu anayetakiwa akupe
viza. Ni muhimu kujifunza kuangalia
matukio kwa jicho la rohoni. Kwasababu
kama hujui waweza kumchukia mtu,
kumbe shetani ndio yupo ndani ya mtu
anayekuzuia. Matendo ya Mitume
10:38 , Shetani anaweza kumuonea mtu,
pia anaweza kumwingia mtu maana
aliwahi kuingia ndani ya Yuda, na wakati
huo usijue kuwa ni shetani kumbe
anatumia mtu. Kabla hujapambana na
mtu anza na rohoni kwanza.
Luka 13:16 “…ambaye shetani
amemfunga…” kumbe shetani anaweza
kumfunga mtu, mapato, ndoto,
matumaini au mafanikio. Unapomtaja
shetani lazima ujue kuwa ana watumishi
wake. Mungu ana watoto wake na
shetani pia ana watoto wake, wale
wanaotenda mapenzi ya shetani ni
watoto wa ibilisi 1Yohana 3:10. Yohana
8:44 “…ninyi ni wa baba yenu ibilisi….”
Wachawi na waganga ni wana wa ibilisi
hivyo hitekeleza kazi za ibilisi duniani,
na hawa ndio wanaoleta matukio
mbalimbali. Shatani hushambulia eneo
ambalo Mungu amekubarikia, ili
usilitumie kukuletea mafanikio kwenye
maisha yako.
Jambo la Muhimu ni kwamba; unatakiwa
uangalie kila tukio linalotokea katika
maisha yako kwa jicho la rohoni, matukio
mengi huanzia kwa wakala wa shetani
na wachawi. Jambo la muhimu ni kuwa
unapookoka unapokea mamlaka dhidi ya
shetani na wakala zake. Ni muhimu
kuchukua nafasi yako kushughulika na
shetani na wakala zake kwa njia ya
maombi (katika ulimwengu wa roho).
Ukifanikiwa kuharibu chanzo cha tatizo
unakuwa umemaliza tatizo asilimia mia
moja.
Sunday, January 27, 2013
MATUKIO YA KICHAWI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment