Na Mch. Kiongozi: Josephat Gwajima
Jumapili 27 th
January 2013
Kuna matukio ambayo yanaweza
kutokea kwenye maisha yako na ukaona
kuwa ni kawaida, lakini tambua kuwa
matukio mengi huanzia rohoni. Matukio
ya kishetani yanayoanzia rohoni
yanaitwa matukio ya Kichawi. Tutajifunza
somo hili kwa kuangalia kwa undani
kuhusu Ayubu. Ayubu 1:1-... ; kitabu
cha Ayubu kinaanza kwa kusema
palikuwa na mtu mmoja katika nchi ya
Usi…. Ayubu alikuwa anamcha BWANA,
si mwenye dhambi…
Shetani akamwambia Mungu
umembariki Ayubu ndio maana
anakucha wewe, Mungu akamwambia,
Katika Mstari wa 12’ “tazama yote
aliyonayo yapo mikononi mwako lakini
usinyooshe mkono juu yake mwenyewe”
jambo la ajabu linatokea, mara tu baada
ya Mungu kumruhusu shetani, jambo la
kwanza shetani alianza kwa kuharibu
mali zake (Ayubu 1:13…). Na katika kila
tukio alilofanya shetani, alibakisha mtu
mmoja wa kumpelekea habari Ayubu.
Hii ni kwasababu shetani alitaka Ayubu
asijue kuwa ni shetani bali Waseba ndio
walioua na kuchukua mifugo wake ili
amuhamishe mtazamo asifahamu kuwa
ni jambo la kishetani,ndivyo amabavyo
shetani anatenda kazi ahata leo.
Tukio la kwanza, Ayubu 1:13-15 Waseba
waliwavamia watumishi wa Ayubu,
unaweza ukawachunguza Waseba katika
mitazamo miwili. Upande mmoja ni
kwamba waseba ni mashetani waliovaa
miili au ni watu walioingiliwa na mapepo
kuharibu wanyama wa Ayubu. Tukio la
pili limetajwa katika mstari wa 16’
kwamba moto ulishuka kutoka
mbinguni, mtoa taarifa anaita moto wa
Mungu, lakini katika kitabu cha (Ufunuo
13:13) inasema shetani anaweza
kushusha moto pia. Huyu mfanya kazi
aliita moto wa Mungu ili kwa njia hiyo
shetani amdanganye Ayubu aache
kuangalia shetani bali awaze kuwa ni
matukio ya kawaida kutokea. Ndio
maana katika waebrani 11:34 , biblia
inasema kwa imani walizima nguvu za
moto, kwasababu kuna moto ambao
waweza kuletwa na shetani. Haijalishi
unapitia moto gani kwenye maisha yako,
moto wa mikosi, kushindwa, umaskini na
kila moto wa maisha yako uzime katika
Jina la Yesu Kristo usiite ni matukio ya
asili.
Tukio la tatu linawahusu Wakaldayo,
katika mstari 17’ wameunda vikosi vitatu
vitatu, nao ni watu ambao
wameandaliwa na shetani ili kutekeleza
yale maongezi ya mwanzo ya Mungu na
shetani. Kumbe ni muhimu kuangalia
matukio kwa namna ya rohoni, liwe
tukio la kukosa umeme au nchi kuwa
maskini liangalie kwa namna ya rohoni.
Nguvu ya shetani ni kukufanya uwaze
kuwa ni tukio la kawaida au la kiasili
lakini kumbe kuna nguvu ya shetani
nyuma yake. Tukio la nne ni upepo
uliotokea na kuangusha nyumba
waliokuwepo watoto wa Ayubu
waliokuwa kwenye sherehe. Cha ajabu
ni kwamba watoto wote wa Ayubu
walikufa kwa maana ndio walikuwa
walengwa,ila Yule mtoa taarifa hakufa
kwasababu si mtoto wa Ayubu na pia
hakuwa amelengwa yeye. Kumbe
unaweza kuwepo mtego wa kichawi nao
unakuwa umemlenga mtu husika, na
ndio maana katika Biblia inataja mitego
ya ibilisi, yaani ibilisi anaweza kumtega
mtu katika kitabu 2Timotheo 2:26
“wapate tena fahamu zao, na kutoka
katika mtego wa ibilisi…..” hivyo alikuwa
anabakishwa mmoja kwasababu lile tego
halimuhusu, maana tego humlenga mtu
au watu husika.
Usione ni kawaida, matukio kama hayo
yanapotokea katika maisha yako, mfano,
unaanza saluni halafu haifanikiwi kumbe
ni kwasababu ya shetani, cha kufanya
unatakiwa uingie rohoni kushughulikia.
Pigo la Ayubu kubwa la kumwekea
majipu katika mwili na magojwa,
unaweza kuhangaika hospitali kama
hujajua kuwa kimeanzia rohoni, hospitali
wataita jipu au cancer lakini kumbe
limeanzia rohoni. Na ndio maana
unaweza kuona meli zinazama hadi
hazionekani kumbe ni kazi za adui
shetani, ni muhimu kujua kila unapoona
matukio duniani kuna matukio ya
kishetani ama yameletwa na shetani au
yamesukumwa kuwepo na shetani. Na
ndio maana ni muhimu unapoingia
kwenye hatari au ajali ukailiitia Jina la
Yesu ambalo ndilo pekee tulilopewa
kuokolewa kwalo.
1Thesalonike 2:18 “ Nalitaka kuja
kwenu….. lakini shetani akatuzuia”
shetani anaweza kumzuia mtu, na mara
nyingi kwenye kuzuia shetani hutumia
watu wa kawaida ili usimtambue.
Huwezi kukutana naye macho kwa
macho kwasababu anatumia waseba,
wakaldayo au upepo. Na ndio maana
unaweza ukawa unataka kusafiri lakini
ukazuiwa na mtu anayetakiwa akupe
viza. Ni muhimu kujifunza kuangalia
matukio kwa jicho la rohoni. Kwasababu
kama hujui waweza kumchukia mtu,
kumbe shetani ndio yupo ndani ya mtu
anayekuzuia. Matendo ya Mitume
10:38 , Shetani anaweza kumuonea mtu,
pia anaweza kumwingia mtu maana
aliwahi kuingia ndani ya Yuda, na wakati
huo usijue kuwa ni shetani kumbe
anatumia mtu. Kabla hujapambana na
mtu anza na rohoni kwanza.
Luka 13:16 “…ambaye shetani
amemfunga…” kumbe shetani anaweza
kumfunga mtu, mapato, ndoto,
matumaini au mafanikio. Unapomtaja
shetani lazima ujue kuwa ana watumishi
wake. Mungu ana watoto wake na
shetani pia ana watoto wake, wale
wanaotenda mapenzi ya shetani ni
watoto wa ibilisi 1Yohana 3:10. Yohana
8:44 “…ninyi ni wa baba yenu ibilisi….”
Wachawi na waganga ni wana wa ibilisi
hivyo hitekeleza kazi za ibilisi duniani,
na hawa ndio wanaoleta matukio
mbalimbali. Shatani hushambulia eneo
ambalo Mungu amekubarikia, ili
usilitumie kukuletea mafanikio kwenye
maisha yako.
Jambo la Muhimu ni kwamba; unatakiwa
uangalie kila tukio linalotokea katika
maisha yako kwa jicho la rohoni, matukio
mengi huanzia kwa wakala wa shetani
na wachawi. Jambo la muhimu ni kuwa
unapookoka unapokea mamlaka dhidi ya
shetani na wakala zake. Ni muhimu
kuchukua nafasi yako kushughulika na
shetani na wakala zake kwa njia ya
maombi (katika ulimwengu wa roho).
Ukifanikiwa kuharibu chanzo cha tatizo
unakuwa umemaliza tatizo asilimia mia
moja.
Sunday, January 27, 2013
MATUKIO YA KICHAWI
Saturday, January 26, 2013
MSIPOONGOKA NA KUWA KAMA VITOTO,HAMTAINGIA KAMWE KATIKA UFALME WA MBINGUNI. ( Mathayo 18 : 3 )
BWANA YESU ASIFIWEE.......
Nakukaribisha mpendwa katika Kristo
Yesu,tujifunze kwa pamoja kuuhusu
ujumbe huu wa leo,Na umekujia muda
sahihi kabisa ungali U mzima wa afya.
Nependa kutambua uwepo wa Roho
mtakatifu muda huu,Ninamualika Yeye
Roho wa Bwana achukue nafasi,ashuke na
uweza wake ili uelewe pindi usomapo
ujumbe huu,maana Yeye ndie mwalimu
wetu siku ya leo.
Hayo maneno yaliyobeba kichwa cha somo
letu ni maneno ya Bwana Yesu Kristo
alipokuwa anawaambia wanafunzi wake, Na
ni maneno ya msingi katika mchakato wa
kwenda mbinguni,Sasa twaweza kusoma ;
Mathayo 18 : 1-3
“ Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu
wakisema,
Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa
mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka
katikati yao,
akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka
na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe
katika ufalme wa mbinguni. ”
Waingiao katika ufalme wa mbinguni ni
wale wenye kufanana kama watoto
wadogo,maana hawa watoto siku zote wao
ni wanyenyekevu sana.
Kumbuka ;
Bwana Yesu Kristo alikuwa anaongea na
wanafunzi wake,wale ambao waliitao Jina
lake,wenye hofu na Mungu,Labda kwa leo
niseme Yesu anazungumza na wewe
uliyeokoka akikuambia USIPOONGOKA NA
KUWA KAMA MTOTO
MDOGO,HAUTAINGIA KAMWE KATIKA
UFALME WA MBINGUNI..
Yaani ingawa umeokoka lakini bado
kuokoka kwako hakukusaidii kuingia katika
ufalme wa mbinguni kama usipoongoka.
• JE KUONGOKA NI NINI ?
• JE KUNA TOFAUTI GANI KATI YA
KUONGOKA NA KUOKOKA ?
MAJIBU ;
Kuongoka ni kugeuka kwa mwenendo wako
wa kwanza na kufuta mwenendo mpya
baada ya kusikia neno la Mungu.
Tofauti kati ya kuongoka na kuokoka ni hii;
• Kuongoka sio NEEMA ya Mungu kwa yule
aliyeongoka,Bali ni jitihada zake pindi
anapoukulia wokovu. Baada ya kuokoka.
• Bali Kuokoka ni KIPAWA/NEEMA ya
Mungu mwenyewe kwa watu wake, Hapa
tunasoma Waefeso 2 : 8-9
“ Kwa maana mmeokolewa kwa neema,
kwa njia ya imani; ambayo hiyo
haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha
Mungu;
wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije
akajisifu. ”
Haleluyaa…
Sasa unaweza ukawa umeokoka lakini
haujaongoka,Yaani umepewa neema ya
kumkiri Bwana Yesu Kristo, kuwa Bwana na
mwokozi wa maisha yako,na kuitwa
MLOKOLE katika jamii ulipo werwe,
lakini ujabadilika matendo yako yale ya
mwanzo kabla ya kuokoka yaani kama ni
WIZI unaufanya kidogo chini kwa chini,au
kama ni UZINZI pia unaufanya chini kwa
chini,na MTU YEYOTE WA NAMNA
HII,HUYO BADO HAJAONGOKA NA KAMWE
HATAINGIA KATIKA UFALME WA
MBINGUNI.
Mfano wa kuongoka;
Tumtizame mtume Paulo namna
alivyokuwa kabla ya kuongoka;
MATENDO 22 : 1-4
“ Enyi wanaume, ndugu zangu na baba
zangu, nisikilizeni, nikijitetea mbele yenu
sasa.
Waliposikia kwamba anasema nao kwa
lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza;
akasema,
Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso,
mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu,
miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria
ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa
jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote
mlivyo leo hivi;
nikawaudhi watu wa Njia hii hata kuwaua,
nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume
na wanawake. ”
Hapo Paulo anasimulia kwa kujitetea
akiwaambia Wayahudi namna
alivyokuwepo hapo awali,lakini pindi
alipookolewa na Bwana Yesu na kutengwa
kwa dhumuni maalumu la kuwa mtume na
mjumbe wa Yesu Kristo,Ndipo
akaongoka,yaani akabadili ule mwenendo
wake wa awali wa kuwahudhi wakristo,na
kuwa mpya kwa ajili ya kazi ya Bwana.
Sasa siku hizi kuna kundi kumbwa la watu
waliokoka kama fasion lakini
HAWAJAONGOKA NA KUWA KAMA
WATOTO WADOGO na watu hayo
nawatangazia kwamba HAWATAUONA
UFALME WA MBINGUNI.
JE NI KWA NINI BWANA YESU ATUMIE
MFANO WA WATOTO KATIKA KUONGOKA?
MAJIBU ;
Kwa sababu watoto wadogo ni wale wenye
KUTII ,na sifa kama,na kuwa na sifa kama
zifuatazo ;
• Watoto wadogo usikia na kushika kile
wanachoambiwa bila kuhoji hoji
• Watoto wadogo hucheza na wenzao kwa
kushirikiana bila kuulizana kabila zao wala
hata majina yao .MFANO ;
wanapocheza wote wanakuwa ni wamoja
watoto wa masikini na watoto wa tajiri
huwezi kuwatofautisha pindi wachezapo.
• Hawapendi makuu,MFANO UNAWEZA
KUMWAMBIA SHUKA KWENYE KOCHI NA
UKAE CHINI,NAYE HUKAA MUDA ULE ULE.
• Watoto wadogo HUPENDANA wana
upendo mzuri
• Hawashikilii mambo Mfano WANAWEZA
KUGOMBANA WAO KWA WAO NA GAFLA
UKIPITA MUDA MDOGO TU,WANAKUWA
PAMOJA WAKICHEZA hawashikilii hasira.
• Watoto wadogo wana DHAMILI
SAFI,ISIYOKUWA NA HATIA Mfano MTOTO
WA KIKE ANAWEZA KULALA MPAKA
ASUBUHI NA MTOTO WA KIUME BILA
KUFANYA CHOCHOTE TENA HATA
WAKILALA UCHI,AU HATA KAMA
WATAKWENDA KUOGA PAMOJA WAO NI
SAWA TU maana dhamila zao zi safi mbele
za Mungu. N.K
Sasa mtu asipo GEUKA na kuwa na TABIA
kama hizo za watoto wadogo KAMWE
HAWEZI KUINGIA KATIKA UFALME WA
MBINGUNI.
JE WEWE UME UKOKA NA KUONGOKA ?
-Au umeokoka bila kuongoka ?
-Au umengoka bila kuokoka ?
Watu wa DINI wao wanaweza kuwa
wameongoka,na kufuata amri na sheria za
dini zao lakini HAWAJAOKOKA na hawana
mpango wowote wa kuokoka na
wakijidanganya kuwa DINI zao kwamba
zitawapeleka mbinguni,au kwa kuongoka
kwao,
Mimi leo ninakutangazia Kuongoka kwa
DINI yako KAMWE HAKUKUINGIZI
MBINGUNI BILA KUOKOKA
KWANZA,ukishaokoka ndipo mchakato wa
kuongoka unafuata.
Na yule aliyeokoka ,asipoongoka KAMWE
HAWEZI KUINGIA KATIKA UFALME WA
MBINGUNI
Mfano ;
Tazama wanafunzi wa Yesu ,wao walokuwa
wameshaokoka,Lakini bado Yesu Kristo
anawaambia na kuwasisitiza WAONGOKE.
( Mathayo 18 : 1-3 )
Haleluyaaa..
Kumbuka ;
Mchakoto wa kwenda mbinguni kwanza
UOKOKE kisha ufanye kuukulia wokovu
yaani KUONGOKA
Ukishaokoka ndipo unafanya mazoezi ya
kugeuka kabisa kwa mwenendo wako wa
kwanza na hapo ikiwa utafanya hiyo
utafanana na mtoto mdogo.
NI OMBI LANGU KWAKO,
KWAMBA KUONGOKA /KUBADILI
MWENENDO WAKO WEWE WENYEWE
HAUWEZI BILA MSAADA WA YESU KRISTO
ULLIYEMPOKEA,
SASA UMSIHI SANA MUNGU AKUPE
UJASIRI NA UWEZO KUACHA KILA JAMBO
BAYA NAYE ATAKUGEUZA UWE MALI
YAKE .
UBARIKIWE.
SHERIA YA DHAMBI
UTANGULIZI:
Warumi 8:1-2 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.” Katika huu mstari wa pili tunaona sheria tatu ambazo Biblia inazitaja, kwanza sheria ya uzima, sheria ya dhambi na sheria ya mauti. Dunia hii inaongozwa na sheria (principles) na ndio maana kuna katika ulimwengu wa kawaida kuna sheria mbalimbali. Mfano sheria ya mvutano (gravitation force) na ndio maana ukichukua jiwe ukalirusha juu litakwenda lakini baada ya muda litarudi chini tena. Na kimsingi huwezi kubishana na sheria hiyo, na ukitaka kuibishia jaribu kwenda gorofani ujirushe lazima utaanguka chini sio kwasababu huna upako bali ni kwasababu ya sheria ya mvutano inayovuta vitu kuja chini.
DUNIA YA KAWAIDA NA SHERIA ZILIZOPO: Kwa kawaida sheria huwa hazibadiliki, kwa mfano sheria inayosema unavyopanda kwenda juu baridi linaongezeka, hii sheria haibadiliki na ndio maana katika mlima kuna baridi zaidi kwasababu ya sheria ambazo zipo. Na vilevile sheria tulizoziona katika Biblia (warumi 8:2) ni bayana yaani hazitanguki. Na kwa maana hiyo hata nchi ili iwe na amani ni lazima ziwepo sheria na kanuni. Na ili watu wafuate sheria wamewekwa polisi, mahakama na magereza kwaajili ya kuhakikisha zile sheria zinafuatwa.
Unapofanya kosa lolote, unaingia kwenye matatizo kwasababu ya sheria iliyopo, kwa namna hiyo polisi watakukamata na kukupeleka mahakamani unapogundulika una makosa unafungwa, hii yote ni kwasababu ya sheria iliyopo.
MAISHA YA KIROHO NA SHERIA YA UZIMA, DHAMBI NA MAUTI: Kama tulivyoona sheria za nchi zinazosimamia maisha ya wananchi ndivyo sheria hizi za rohoni zinavyotenda kazi. Kimsingi unapovunja sheria ile sheria inakushusha chini bila ya wewe kujua. Na ndio maana biblia inasema “kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele” Kuna tofauti kati ya mshahara na zawadi, kwasababu unapotenda kazi ni lazima upokee mshahara wake, upende usipende na ulieusilie.
Kimsingi, wewe unaweza ukawa unatenda vitu na hakuna anayekuona, unaweza ukawa umeokoka lakini unatenda mambo mabaya au dhambi katika ulimwengu wa siri. Siku utakayopokea mshahara kila mtu atajua isipokuwa hatojua umepokea hilo kutoka katika kazi dhambi gani uliyotenda. Unaweza kumuona mtu alikuwa wa Mungu lakini akafa ghaflaghafla watu wakasikitika na kumbe umepewa mshahara wa matendo yake ya sirini. Maisha yako ya sirini ni muhimu sana.
SHERIA YA DHAMBI:
Warumi 6:23: “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Ezekieli 18:4: “Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa.”
Nini maana ya maneno haya?; hapo mwanzo sheria alikuwa mbinguni, akifikia kipindi akafanya yaliyomaovu na kuasi hivyo akafukuzwa mbinguni. Na alipotupwa duniani akaanzisha utawala wake katika kila mtaa wa dunia hii ili kutenda kazi kila mahali. Haya majeshi ya pepo wabaya yapo kwaajili ya kuwapa watu mishahara ya matendo mabaya wanayoyatenda.
Kwasababu shetani alikuwa mbinguni, anaifahamu biblia anajua kanuni za Mungu, hivyo, unavyotenda lililoovu shatani anajua kuwa umekosea na amekaa tayari kugawa mshahara. Kumbe mshahara huu hautoki kwa Mungu bali shetani ndiye alipaye. (Yohana 10:10) yaani shetani hatendi kazi isipokuwa kuharibu, kuchinja na kuharibu. Unapotenda uovu kwa siri, mashetani hukaa mahali ili kugawa mshahara wa uovu ile. Na kwa muda ambao mashtaka yapo na hayajakanushwa kwa kutubu, mtu huyo atajikuta anafia dhambini. Kwa namna hiyo watu wengi wanaishi kwenye magonjwa na matatizo yanayotokana na maisha yao ya sirini ambayo hakuna anayejua.
Kiukweli hakuna dhambi ndogo wala kubwa, hivyo dhambi iliyondogo sana yaweza kumpeleka mtu Jehanamu. Dhambi ambazo watu huzidharau na kuziita ndogo ndizo zipelekazo watu Jehanamu bila hata ya wao kujua. Jifunze kutubu kila unapojikuta unamkosea Mungu.
Ni muhimu kutafuta mahali ulipouacha upendo wako wa kwanza, uhurudie na ukatubu. Mungu ni mwenye rehema atakusamehe kabisa na hatoyakumbuka makosa yako tena. Tengeneza maisha yako ya rohoni.
Wednesday, January 23, 2013
UPINZANI UNAPOTOKEA KUPINGA UAMSHO NA WOKOVU, BIBLIA INAKUSHAURI UFANYE NINI?
Mara nyingi upinzani unaotokea unakuwa katika maeneo ya kupinga uamsho, kupinga wokovu, kupinga mafundisho ya kweli, kupinga miujiza ya kweli ya Mungu inayotokea na pia, kuwapinga watumishi wa Mungu wanaotumiwa na Mungu katika uamsho.
Katika jibu la swali la mwezi huu ningependa nikuwekee mistari mbalimbali kutoka katika Biblia inayotushauri tuwe tunafanya nini unapotokea upinzani dhidi ya uamsho.
Ni vizuri kujua ya kuwa si kila mtu anakubaliana na mambo ya uamsho, pia si kila dhehebu la kikrsto linakubaliana na uamsho wa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo ni vizuri ujiandae na ujue cha kufanya unapokutana na upinzani.
Unaposongwa na upinzani Biblia inakushauri ufanye yafuatayo:
1. FURAHI WALA USIKASIRIKE! (Mathayo 5:11,12; I Petro 4:12-16):
"Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi, na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili (ya Yesu) yangu. Furahini na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu’’.
‘’Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoshiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine. Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo (au ikiwa kwa sababu ameokoka) asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo”.
2. BARIKI WALA USILAANI! (Warumi 12:14; Luka 6:28, I kor 4:12,13)
"Wabariki wanaowaudhi, barikini, wala msilaani pia, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi’’.
Mtume Paulo akiwaandikia Wakorintho jinsi wao walivyofanya anasema; “tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twastahimili; tukisingiziwa twasihi’’.
Na wewe fanya kama Mtume Paulo ukitukanwa kwa sababu ya kuokoka bariki, ukiudhiwa kwa sababu ya wokovu stahimili au vumilia, ukisingiziwa uongo, jifunze kujibu kwa hekima!
3. TENDA WEMA USILIPIZE KISASI! (Warumi 12:17,18; Waebrania 12:14,15; Warumi 12:19-21; Luka 6:27
"Msilipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo’’.
‘’Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu(mwachie Mungu jambo hilo linalokuletea hasira); maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu mimi, mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema’’.
‘’lakini nawaambia ninyi mnaosikia wependeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi.’’
4. WAOMBEE WANAOWAUDHI! Luka 6:28b; Mathayo 5:43-45, Mathayo 26:41)
‘’Waombeeni wale ambao wawaonea ninyi’’. ‘’Mmesikia kwamba menenwa, umpende jirani yako, na umchukie adui yako, lakini mimi (Yesu) awaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi; ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki’’.
“ Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribu; roho ii radhi, lakini mwili ni dhaifu’’.
5. USIKATISHWE TAMAA ENDELEA KUFANYA ANALOKUAMBIA MUNGU KATIKA UTII NA HEKIMA! (Warumi 16:17-19)
‘’Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza (ya kweli); mkajiepushe nao. Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu. Maana utii wenu umewafikilia watu wote… lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya. Naye Mungu wa amani atamseta shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi’’.
6. WASHIRIKISHE WATEULE WENZAKO WAKUOMBEE KATIKA UPINZANI UNAOKUZUNGUKA! (Warumi 15:30-32).
Ndivyo Mtume Paulo alivyofanya alipowaandikia wateule wenzake aliposema;
‘’Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu; kwamba niokolewe na wale wasioamini katika Uyahudi, na tena huduma yangu niliyo nayo huko Yerusalemu ikubalike kwa watakatifu; nipate kufika kwenu kwa furaha kama apendavyo Mungu, nikapate kupumzika pamoja nanyi’’.
Yamkini Mungu atajibu maombi ya wateule hao wakiomba kwa imani na kwa bidii juu yako. Kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya 12 kinatueleza jinsi ambavyo Mtume Petro alipokumbwa na upinzani hata akafungwa-lakini (Kanisa) wenzake waliokoka waliomba kwa juhudi kwa ajili yake na Mungu akamfungua toka gerezani.
7. JIEPUSHE NA MABISHANO! (Tito 3:9; Wakolosai 4:5)
Mara nyingi upinzani wa wokovu na mambo ya uamsho unapotokea-kunatokea pia maswali na mabishano yasiyokuwa na msingi wala maana yoyote. Wengi bila kujua wamejikuta wameingia katika majibizano na mabishano juu ya wokovu na neno la Mungu. Biblia inasema hivi:
‘’Lakini maswali ya upuuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria (Neno la Mungu). Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana’’ enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu’’.
8. USIKATE TAMAA, VUMILIA MPAKA MWISHO! (I Petro 3:13-17; Mathayo 24:13)
‘’Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema? Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu’’.
Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo. Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya’’. ‘’lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka’’.
9. USIONE HAYA- SONGA MBELE KATIKA WOKOVU (Waebrania 12:1-3; I Petro 4:15,16)
‘’Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu’’. ‘’Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine. Lakini ikiwa kwa sababu ni mkristo (au ameokoka) asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo’’.
10. USIJIULIZE – ULIZE UTAKACHOJIBU! (Marko 13:9,11)
‘’Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa;; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili (ya Yesu), kuwa ushuhuda kwao …. Na watakapowachukuwa ninyi, na kuwasaliti, msitafakari kwanza mtakavyosema, lakini lolote mtakalopewa saa ile, lesemeni; kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu’’.
11. MUWE NA KIASI NA KUKESHA! (I Petro 5:8-9; Yakobo 1:2-4; Yakobo 4:7; I Petro 5:10)
‘’Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka – zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani…’’ ‘’Ndugu zangu, hesabuni yakuwa ni furaha tupu, mkiangikia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi (uvumilivu). Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno’’. ‘’Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani, naye atawakimbia’’.
“ Na Mungu wa neema yote aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu’’.
Monday, January 21, 2013
Sunday, January 20, 2013
Saturday, January 19, 2013
KWANINI UNASHINDWA KUMTUMIKIA MUNGU ???
Na Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima.
Kuna swali ambalo kama mtu uliyeokoka unatakiwa ujiulize kila siku, yaani “kama ikitokea leo umekufa una kitu gani cha kumwonyesha Mungu?” ukisoma Danieli 12:3 inaeleza kuwa, Wale Waliowaongoza wengi kutenda mema watang’aa kama nyota siku ya mwisho. Hawa ni watu wanaomtumikia Mungu, kumbe siku ya mwisho tutarudi mbinguni kila mtu atatoa hesabu yake. Lakini kama ulimtumikia Mungu duniani, utang’aa kama nyota.
Kwenye Biblia hata polisi walimtumikia Mungu. Esta 3:1-6 Modekai alikuwa anafanya kazi katika nyumba ya mfalme yaani alikuwa anakaa kwenye lango la mfalme. Kumbe kuna uwezekano wa kuwa polisi na huku unamtumikia Mungu. Uwezekano huo upo.
- Atabariki chakula chako:- hapa hata kama utakula chakula chenye sumu, hauwezi kudhurika kwasababu unamtumikia Mungu.
- Atabariki maji yako:- vilevile atabariki maji yako, yaani hayatakudhuru.
- Nitakuondolea magonjwa kati yako:- ukimtumikia Mungu, huwezi kuingia katika magonjwa yaani kama ulikuwa unaumwa Mungu atakuponya kwa vile unamtumikia Mungu.
- Hautakuwa mwenye kuharibu mimba:- Kuharibu mimba maana yake unaanza kitu, lakini kabla hakijafanikiwa kinaharibika. Inaweza ikawa mimba au hata kampuni.
- Kutokuwa tasa:- kama unamtumikia Mungu hata kama una miaka mingi unaweza kuzaa. Alikuwepo Sara ambaye alizaa akiwa na miaka 90 pamoja yakuwa umri ulikuwa umeendelea sana.
- Mungu atatimiza hesabu za siku zako:- unapomtumikia Mungu, atakupa miaka mingi ya kumtumikia Mungu, yaani kwasababu unafanya kazi yake duniani Mungu anakuongezea miaka ili umtumikie vizuri. Maana hata Mfalme Hezekia alipoumwa alimkumbusha Mungu jinsi alivyomtumikia Mungu, na Mungu akamwongezea miaka kumi na tano asingeweza kupata kwa maombi tu bali ni kwa kumtumikia Mungu.
- Mungu atatuma utiisho wake ukutangulie:- yaani huu ni uungu wa Mungu juu ya maisha ya mtu.
- Mungu atawafadhaisha wale watakaokufikiria.
- Mungu atawafanya adui zako wakuonyeshe maungo yao.
- Mungu atatuma mavu mbele ya adui zako wote.
- Mungu atawafukuza aduiazako wote.
Unaweza ukamtumikia Mungu huku ukiwa na nafasi katika uongozi au unafanya kazi nyingine yoyote. Alianza kuwa kama mbunge ingekuwa siku zetu lakini pamoja na huo uongozi aliweza kumtumikia Mungu. Danieli 2:48; kwa habari ya Danieli tunagundua kuwa kuna uwezekano wa kumtumikia Mungu huku ukiendelea na kazi yake. Kumbe kumtumikia Mungu Danieli 5:25-29; unaweza kumtumikia Mungu katika kiwango cha juu na bado ukafanya kazi zako za kawaida kama Danieli. Danieli 6:48:- hata kipindi cha Mfalme Koreshi, Danieli aliendelea kustawi, kwasababu alimtumikia Mungu.
JE !!! UMEJIANDAAJE KUKUTANA NA MUNGU ???
Tukumbuke kwamba haipo nafasi ya kurudi duniani, ili tutubu ukifa ni basi.
Wapo watu wengi wanaongoza makanisa makubwa sana kwa umati mkubwa na huku wakiabudu sanamu.
Ibada ya sanamu haiwezi kuokoa bali ni YESU pekee awezaye kuokoa, na nje yake hakuna mwingine aokoaye. anawapenda wenye dhambi, lakini anachukia dhambi.
NI WAKATI WAKO KUCHUKUA HATUA SASA KUJIANDAA KUKUTANA NA MUNGU.
FIKIRI ikiwa unapata nafasi ya kukutana na MUNGU sasa hivi UTAMWAMBIA NINI ??????
" !!! CHUKUA HATUA SASA !!! "
Tuesday, January 15, 2013
MKRISTO NA UTANDAWAZI
Neno utandawazi au globalization lina
maana nyingi sana kutegemea na matumizi
yaloyokusudiwa...
Maan ya kawaida(People's
philosophy).....Utandawazi ni mfumo wa
kuifanya dunia iwe kama kijiji kimoja kwa
mfumo wa
mawasiliano,teknolojia,mtandao,siasa,uchumi
na utamaduni....
Maana ya Kiblia(Mtazamo wa kikristo-
Christian philosophy),Utandawazi ni
harakati za mfumo mpya wa kidunia ambao
utaongozwa na mpinga kristo unawezesha
watu wa dunia kuwa na uchumi
mmoja,siasa moja,tamaduni moja,dini
moja,sarafu moja,rais mmoja,na teknolojia
moja..Ufunuo 13:16-18
Kulingana na maandiko,utandawazi ulioko
leo ni maandalizi tu ya mfumo mpya ujao
wa mpinga Kristo 2The 2:6-10
Dalili ya mfumo huo mpya ni nyingi
ikiwemo kuongezeka kwa maarifa na kasi
ya utendaji isiyo ya kawaida ya
binadamu..Daniel 12:4
MADHARA YA UTANDAWAZI KWA
KANISA...
1.Wakristo wengi wamevutwa na dunia na
wametokea kuipenda dunia kuliko
Mungu..kwani wanaona matunda ya
utandawazi ni matamu..1Yoh 2:15-17
2.Mmonyoko wa maadili makanisani
3.Kanisa limekuwa la kisasa mno
4.Miziki ya dunia inawavuta waliookoka
KUJILINDA NA UTANDAWAZI
1.Chagua marafiki wazuri
2.Kutii neno la Mungu...
Tuesday, January 8, 2013
KWANINI SI RAHISI KUTENDA MEMA?
Kwa Nini Si Rahisi Kutenda Mema?
SAULI alipofanya mabaya, ni nani aliyefurahi?— Ni Shetani Ibilisi. Hata viongozi wa dini ya Wayahudi walifurahi pia. Kisha Sauli alipogeuka na kuwa mwanafunzi wa Mwalimu Mkuu na kuitwa Paulo, viongozi hao wa dini walianza kumchukia. Kwa hiyo unaelewa kwa nini si rahisi mwanafunzi wa Yesu kutenda mema?—
Wakati mmoja kuhani mkuu Anania aliwaambia watu wampige Paulo usoni. Anania hata alijaribu kumfunga Paulo gerezani. Paulo aliteswa sana alipogeuka na kuwa mwanafunzi wa Yesu. Kwa mfano, watu wabaya walijaribu kumwua Paulo kwa kumpiga kwa mawe makubwa.—Matendo 23:1, 2; 2 Wakorintho 11:24, 25.
Watu wengi watajaribu kutufanya tutende mambo yanayomchukiza Mungu. Kwa hiyo swali ni: Unapenda mema kwa kadiri gani? Je, unapenda mema sana hivi kwamba utayatenda hata kama wengine watakuchukia? Unahitaji ujasiri kufanya hivyo, sivyo?—
Lakini labda unajiuliza, ‘Kwa nini watu watuchukie kwa kufanya mema? Je, hawapaswi kufurahi badala yake?’ Inafaa iwe hivyo. Mara nyingi watu walimpenda Yesu kwa sababu ya mambo mazuri aliyoyafanya. Wakati mmoja watu wote mjini walikusanyika mlangoni mwa nyumba ambayo Yesu alikuwa anakaa. Walikuja kwa sababu Yesu aliwaponya wagonjwa.—Marko 1:33.
Lakini wakati mwingine watu hawakupenda mambo ambayo Yesu alifundisha. Ijapokuwa alifundisha yaliyo kweli, watu wengine hawakupenda mafundisho hayo. Wengine hata walimchukia sana kwa sababu ya kusema mambo ya kweli. Ilikuwa hivyo siku moja huko Nazareti, ambako Yesu alilelewa. Aliingia ndani ya sinagogi, mahali ambapo Wayahudi walikuwa wanakutania ili kumwabudu Mungu.
Yesu akatoa hotuba nzuri kutoka kwa Maandiko akiwa huko. Mwanzoni, watu walipenda sana hotuba hiyo. Wakastaajabia maneno mazuri aliyoyasema. Hata hawakuamini kwamba huyo ni yule kijana ambaye amekulia jijini mwao.
Lakini Yesu akasema jambo jingine. Akataja wakati ambapo Mungu aliwapendelea watu ambao hawakuwa Wayahudi. Yesu aliposema hivyo, wale waliokuwa katika sinagogi wakakasirika. Unajua sababu?— Walifikiri kwamba ni wao tu ndio wanaopendelewa na Mungu. Walifikiri kwamba wao ni bora kuliko watu wengine. Kwa hiyo wakamchukia Yesu kwa kusema hivyo. Unajua walijaribu kumfanyia nini?—
Biblia inasema: ‘Walimshika Yesu na kuharakisha kumtoa nje ya jiji. Wakampeleka hadi ukingo wa mlima ili wamwangushe chini na kumwua! Lakini Yesu akapita katikati yao na kwenda zake.’—Luka 4:16-30.
Kama hali hiyo ingekupata, je, ungethubutu kurudi na kuzungumza na watu hao kumhusu Mungu?— Ungehitaji ujasiri kufanya hivyo, sivyo?— Hata hivyo, baada ya mwaka mmoja hivi, Yesu alirudi Nazareti. Biblia inasema: “Akaanza kuwafundisha katika sinagogi lao.” Yesu hakuacha kusema kweli eti kwa sababu ya kuwaogopa wanadamu ambao hawakumpenda Mungu.—Mathayo 13:54.
Siku nyingine wakati wa sabato, Yesu alikuwa mahali fulani na pakawa na mtu mwenye mkono uliokuwa umenyauka au kulemaa. Yesu alikuwa na nguvu za Mungu za kumponya mtu huyo. Lakini baadhi ya watu waliokuwapo walijaribu kumfadhaisha Yesu. Mwalimu Mkuu angefanya nini?— Kwanza akauliza: ‘Kama ungekuwa na kondoo mmoja naye aanguke ndani ya shimo siku ya Sabato, je, ungemwondoa shimoni?’
Bila shaka, wangemwondoa kondoo shimoni hata kama ni siku ya Sabato, siku ambayo walipaswa kupumzika. Basi Yesu akasema: ‘Ni bora kumsaidia mtu siku ya Sabato, kwa sababu mtu ni bora kuliko kondoo!’ Ilikuwa wazi kwamba Yesu alihitaji kumsaidia mtu huyo kwa kumponya.
Basi Yesu akamwambia mtu huyo anyoshe mkono wake. Mara tu mkono wake ukaponywa. Mtu huyo alifurahi sana. Lakini namna gani wale watu wengine? Je, walifurahi?— La. Wakamchukia Yesu hata zaidi. Wakatoka nje na kufanya mipango ili wamwue!—Mathayo 12:9-14.
Hivyo ndivyo ilivyo leo. Hata tufanye nini, hatuwezi kuwapendeza watu wote. Kwa hiyo ni lazima tuamue ni nani tunayetaka kumpendeza hasa. Ikiwa ni Yehova Mungu na Mwanaye, Yesu Kristo, basi ni lazima kila wakati tufanye vile wanavyotufundisha. Lakini tukifanya hivyo ni nani atakayetuchukia? Ni nani atakayefanya iwe vigumu kwetu kufanya yaliyo mema?—
Shetani Ibilisi atatuchukia. Lakini ni nani mwingine atakayetuchukia?— Ni wale ambao wamedanganywa na Ibilisi kuamini uwongo. Yesu aliwaambia viongozi wa dini wa siku zake hivi: “Ninyi mmetoka kwa baba yenu Ibilisi, nanyi mnataka kufanya tamaa za baba yenu.”—Yohana 8:44.
Kuna watu wengi wanaopendwa na Ibilisi. Yesu anawaita “ulimwengu.” Unafikiri “ulimwengu” ambao Yesu anazungumzia ni nini?— Hebu tuone Yohana sura ya 15, mstari wa 19. Hapo tunasoma maneno haya ya Yesu: ‘Kama mngekuwa sehemu ya ulimwengu, ulimwengu ungependa sana kilicho chake. Sasa kwa sababu ninyi si sehemu ya ulimwengu, bali nimewachagua ninyi kutoka ulimwenguni, ulimwengu unawachukia ninyi.’
Kwa hiyo, ulimwengu ambao unawachukia wanafunzi wa Yesu unatia ndani wale wote wasiokuwa wanafunzi wake. Kwa nini ulimwengu unawachukia wanafunzi wa Yesu?— Fikiria jambo hilo. Ni nani mtawala wa ulimwengu huu?— Biblia inasema: “Ulimwengu mzima unakaa katika nguvu za yule mwovu.” Mwovu huyo ni Shetani Ibilisi.—1 Yohana 5:19.
Unaona sasa ni kwa nini si rahisi sana kutenda mema?— Shetani na ulimwengu wake wanafanya iwe vigumu. Lakini kuna sababu nyingine. Unakumbuka ni sababu gani?— Katika Sura ya 23 ya kitabu hiki, tulijifunza kwamba sote tumerithi dhambi. Je, halitakuwa jambo zuri ajabu wakati dhambi, Ibilisi, na ulimwengu wake hautakuwapo?—
Biblia inaahidi: “Ulimwengu unapitilia mbali.” Hii inamaanisha kwamba wale wote ambao si wanafunzi wa Mwalimu Mkuu hawatakuwapo tena. Hawataruhusiwa kuishi milele. Je, unajua ni nani watakaoishi milele?— Biblia inaendelea kusema: “Yeye anayefanya mapenzi ya Mungu anadumu milele.” (1 Yohana 2:17) Ndiyo, ni wale tu wanaofanya mema, wanaofanya “mapenzi ya Mungu,” ndio watakaoishi milele katika ulimwengu mpya wa Mungu. Kwa hiyo, hata kama si rahisi, tunataka kufanya mema, sivyo?—
Tusome pamoja maandiko haya yanayoonyesha ni kwa nini si rahisi kufanya yaliyo mema: Mathayo 7:13, 14; Luka 13:23, 24; na Matendo 14:21, 22.